zanglassworks

AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, December 5, 2013

Afatae mkumbo hana safari

Mhe. Mansour Yusuf Himid, aliyekuwa mwakilishi wa jimbo la Kiembesamaki kabla ya kuvuliwa uanachama wa CCM
Mhe. Mansour Yusuf Himid, aliyekuwa mwakilishi wa jimbo la Kiembesamaki kabla ya kuvuliwa uanachama wa CCM
Na Abdallah Vuai, Zanzibar
Harakati za uchaguzi mdogo katika jimbo la Kiembesamaki katika Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja zimeanza rasmi wiki iliyopita, Chama cha Mapinduzi tumeona wanachama wake mwameanza kupigana vikumbo kwenye ofisi za Chama hicho wakichukua fomu za kuwania ujumbe wa baraza la Wawakilishi kupitia jimbo hilo.
Uchaguzi mdogo katika jimbo hilo unafanyika baada ya CCM kumfuta uanachama, Mansoor Yussuf Himd aliekuwa mwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki kwa madai ya kwenda kinyume na sera msimamo wa Chama hicho kuhusu suala zima la mfumo wa muundo wa Muungano.
Tafauti na uchaguzi mwengine, katika uchaguzi wa Jimbo hili,ushindani utakuwa ni mkubwa baina ya vyama ambavyo vyenye nguvu za kisiasa hapa Zanzibar, CCM na CUF.
Hali hii itawaweka wagombea kwenye joto wakati wote hususan ikitazamwa hali ya ksiaisa ya hivi karibuni.
CCM itakabiliwa na upinzani karibu kila kona, kwanza kuna kundi la wapigakura ambao hawakufurahishwa na uamuzi wa kumfukuza mwakilishi wao, kundi hili linaweza kukiadhibu Chama cha CCM, lakini pia kuna wale ambao wanaunga mkono misimamo ya mwakilishi wao aliyefukuzwa nao sidhani kama wanaweza tena kuwa watiifu kwa Chama chao.
Nadhani pia Chama cha CUF kitatumia turufu yake ya mwaka 2010 kuweza kukiendesha mchakamchaka Chama cha CCM ambacho kwa hali ilivyo katika jimbo hilo kinahitaji kutumia nguvu ya ziada kuweza kutetea kiti chao, vyenginevyo ni mambo magumu kwao.
Matokeo katika la Jimbo la Kiembesamaki yanaweza kutusaidia angalau kuchora picha ya hali ya mambo itakavyokuwa kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 hapa Zanzibar ambapo wapigakura watakuwa ni wapya na wenye matumaini ya maendeleo zaidi kuondolewa matatizo yao ya kiuchumi na ukosefu wa ajira.
Ule wakati wa wapigakura kuchagua hata kumbi umeshatuacha mkono, leo watu wanataka sera na umakini wa utekelezaji wa sera hizo, ubabaishaji hauna nafasi katika medani za siasa hapa Zanzibar.
Tukijiandaa kuelekea kwenye kampeni hapo baadae kidogo, kunan masuala ambayo yanahitaji kupigiwa chapuo, nayo ni elimu kwa wapigakura maana katika uchaguzi mara nyingi zile zilizopita kuanzia mwaka 1995 hadi 2010 watu walikubali kupoteza heshima na utu kwa sababu ya kitu.
Tunategemea wapigakura katika Jimbo hili wataweza kufanya maamuzi sahihi juu ya mgombea wanaemtaka, waepukane na kufuata mkombo maana afatae mkumbo hana safari, watazame sera, dhamira ya mgombea na pia kupima kule walikotoka, walipo na wapi wanataka kuelekea katika Jimbo lao.
katika baadhi ya Majimbo, wapo wapigakura wenye uchu wa maendeleo katika Majimbo yao ambao hawataki tena kusikiliza nyimbo zenye kuwalaza usingizi huku wao wakibaki kuhesabu miezi na miaka, lakini maendeleo yao ni yale yale ya siku za nyuma.
Wapigakura katika majimbo mengine wameweza kuwaweka roho juu wabunge na wawakilishi wao wasiowajibika kwao, katika majimbo hayo, wapigakura hawakubali tena kugawiwa khanga, vitenge au kupikiwa vyakula kama pilau na vyenginevyo kushawishiwa kumuunga mkono mgombea fulani.
Kura ni silaha, wananchi wa Jimbo la Kiembesamaki hawana budi kuitumia vizuri, wawapime wagombea kwa vigezo, tunategemea kuwasikia wagombea wakizungumzia kwa nia ya kutatua kero za wananchi badala ya matusi, kejeli au kuhubiri chuki, tunawategemea watueleza namna watakavyoweza kuzipatia
Ufumbuzi kero za wananchi
Umefika wakati wapigakura kufahamu kuwa ni wao kwa umoja na nguvu zao ndio zinazomfanya raia mwenziwao kuitwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi, lakini wakae wakijuwa kwamba watakapoona Mwakilishi wanasiasa wengine wakipiga soga na kushindwa kutimiza majukumu yake basi fahamu kuwa wanawatumia wananchi kama ngazi ya kufanikisha mambo yao wenyewe.
tiba sahihi ya tabia ya hii ni kuhakikisha kuwa mgombea wanaetaka kuchaguliwa lazima atimize vigezo vyao na anatimiza wajibu wake na kukidhi haja za wananchi, ni kwa kuwa na viongozi waadilifu.
Ni muhimu wapigakura wa Kiembesamaki wakafahamu kwamba mara nyingi ubora au udhaifu wa Mwakilishi hutokana na maamuzi ya wananchi wenyewe kupitia kwenye uchaguzi kama hapo baadae watakapo piga kura kumchagua katika Jimbo hili.
Kwanini iwe hivyo, jawabu yake ni kwamba baadhi ya wapigakura wamekuwa na hulka ya kupuuza mambo, wanajiandikisha vizuri, lakini siku ya uchaguzi wanadharau, kitendo hichi kinasababisha mgombea dhaifu asiekuwa na uwezo kuweza kushinda katika uchaguzi.
Ni kawaida kuwasikia wapigakura wakisema kwamba kiongozi yeyote atakayechaguliwa kwao ni sawa tu.
Hili ni jambo lisilotakiwa kufanywa, tusidharau kupigakura kwa kutoa vizingizo mbalimbali, mwenendo huu wa baadhi ya wananchi kudharau na kuacha kupiga kura wakati wa uchaguzi  unadumaza demokrasia.
Wananchi wa Kiembesamaki, waache mwenendo huu, tuizike hulka ya kupuuza kupigakura kwani ni udhaifu mkubwa kwetu, kutokwenda kupigakura pia ni sehemu ya dhana potofu na yule ambae anafanya hivyo ajuwe kuwa anachangia kurudisha nyuma juhudi za kukuza demokrasia.
Ijapokuwa halazimiki kufanya hivyo, lakini gharama yake atailipa kwa kipindi cha muda wa miaka mitano. Ni jambo la kushangaza mtu umejiandikisha, kisha unaopuuza kwenda kupiga kura ni kwa faida ya nani, hivi inakuwaje mtu utegemee kupata kiongozi bora bila ya kushiriki kumchaguwa?
Katika Mataifa mengi tunaona jinsi nguvu ya kura katika uchaguzi inavyowaweka viroho juu viongozi na kwa msingi huo kura mara zote zinawalazimisha viongozi kuwaheshimu wapigakura wao.
Utaratibu wa kupigakura katika jamii unafanya kuwepo na uwajibikaji wa moja kwa moja kwa wanaochaguliwa, utaratibu huu unaweka usawa, heshima baina ya wapigakura na mpigiwa kura kwani wale wanaochaguliwa wanaelewa kuwa wananchi ndio wenye mamlaka ya kumpa uongozi yule wamtakae.
Haki ya kupiga kura pia huwapa wananchi nafasi ya kupima na kuchagua viongozi ili kuboresha hali zao na ya nchi kwa jumla. Kwa maana hiyo viongozi waliochaguliwa hujitahidi kuwa karibu na wananchi kwa kutatua matatizo yanayowakabili ili waweze kudumu madarakani.
Katika utaratibu huu haitarajiwi kabisa viongozi walio wababaishaji, wasiowajibika, wenye kibri, kusimama mbele ya hadhira ya wapigakura kuwaomba wawape fursa ya kuwaongoza na wananchi nao wakawapa tena fursa hiyo.
Silaha hii ya kura ikiwa haitatumika vizuri, basi haitasaidia kuwamwaga viongozi wababaishaji katika Majimbo. Matumizi mabaya ya kura ni pale wapigakura wanapopuuza kwenda kupiga kura.
Wengine hawapuuzi kwenda kupiga kura, wanakwenda, lakini kwenda kwao kunasukumwa na vijizawadi wapewavyo na wagombea, aina hii ya wapiga kura mara nyingi huwa radhi kumchaguwa mgombea kwa thamani ya mvao wa khanga,kikoi au kuahidiwa ahadi hewa.
Kura ni muhimu ni kama moyo kwa mwanadamu, mchezo wetu ndio mauti yetu, tujiulize tunafanya uchaguzi kwa kutimiza matakwa ya kisheria tu au tunataka mabadiliko katika Majimbo yetu?
Ni jambo lisilokuwa na ubishi kwamba Viongozi wa kuchaguliwa, ni lazima wawajibike kwa wananchi, bila ya kufanya hivyo, wananchi tuchukuwe maamuzi magumu ya kutowachagua.
Wapiga kura wa Kiembesamaki huu ni wakati wenu, pimeni sera na ahadi za wagombea kwa umakini, epukeni kuondoka patupu, suala la aina gani ya Mbunge mnaemtaka ni la kwenu, si la mwengine.
Chanzo: Mwananchi

No comments :

Post a Comment