Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, December 28, 2013

Dk Salmin: Nilimpenda Gaddafi

Na Mwinyi Sadallah
RAIS wa Zanzibar wa awamu ya tano Dk Salmin Amour ametoa ya moyoni akisema Kiongozi wa Libya, Muammar Gaddafi ni miongoni mwa viongozi wa Afrika ambao walikuwa na upeo wa kuona mbali.
Dk Salmin alisema kifo chake kilikuwa ni hujuma, lakini akasema cha kishujaa kama kilivyo kwa viongozi mahiri duniani, waliyo hujumiwa na mabeberu.
Alisema hayo wiki hii nyumbani kwake Migombani, Zanzibar alipokuwa akizungumzia miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Gaddafi, aliuawa na Wanamgambo wa serikali ya sasa ya Libya, Oktoba 20, mwaka 2011.
“Gaddafi ni mwana wa Afrika aliyekufa kishujaa…kifo chake ni dhulma kama aliyofanyiwa Patrice Lumumba wa Jamhuri ya Demokrasi ya Kongo (DRC),” alisema Dk Salmin.
Alisema kifo cha Gaddafi kilitokana na chuki za Mabeberu wa nchi za Magharibi ambao walichukizwa na uthabiti wa misimamo yake ya kuitetea na kutaka Afrika ijitegemee kiuchumi na kisiasa, ili ifanikiwe kimaendeleo.
Dk Salmin alisema Gaddafi akiwa madarakani alimudu kujenga uchumi imara kwa nchi yake, kuwaletea maendeleo ya haraka watu wake, kujenga makazi bora, kuimarisha huduma za jamii kama afya, maji, barabara na kusomesha wataalamu.
Rais huyo mstaafu wa Zanzibar ambaye ni maarufu kwa jina la Komando alisema: “Itikadi yake ilishiba siha ya uzalendo…alitamani umoja wa Afrika..ni kiongozi aliyeona mbali…aliyejiamini na alilipenda bara la Afrika,”.
Akizungumzia utawala wake uliodumu kwa miaka 10, Dk Salmin alisema alifanikiwa kuivusha Zanzibar katika vikwazo mbalimbali vya kiuchumi.
Alisema uwezo huo ulitokana na uzoefu wake ndani ya Chama cha Afro Shirazi (ASP) na masomo yake ya fani ya uchumi na siasa.
Alisema wakati akiwa madarakani alianzisha mpango wa kuwa na bandari huru, maeneo huru ya uchumi, ili kuifanya Zanzibar, ijitegemee.
“Tokea nikisoma nilipenda somo la biashara…ASP ndiyo iliyonijengea maarifa ya kazi hiyo nikachukua masomo ya siasa na uchumi huko Ujerumani,” alisema Dk Salmin na kuongeza.
“Dhamira ilikuwa ni kujenga uchumi…Nilitaka Zanzibar ipate maendeleo ya kweli na haraka…Nilipoishia wezangu naamini wameendeleza…wakitaka nishauri niko tayari,”.
Akizungumzia miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dk Salmin alisema harakati zake zilitokana na chemchem ya vuguvugu la wana Afrika (PAFMECA) kutaka kujikomboa kutokana na madhila ya kutawaliwa na wakoloni.
Kuhusu jina la Komando, alisema lilitokana na mapenzi ya wananchi wenyewe kutokana na kukubaliana na siasa pamoja na misimamo thabiti aliyokuwa nayo ya kutetea misingi ya ASP na kulinda Mapinduzi, yasivurugwe..


No comments :

Post a Comment