Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, December 29, 2013

Dk. Shein aitaka SUZA kuelekeza mikakati yake kwa maendeleo ya nchi

NA MWANDISHI WETU

29th December 2013


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti waa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, pia Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa SUZA, akisalimiana na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Ali Juma Shamuhuna, wakati alipowasili chuoni hapo.
Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein ameutaka uongozi wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) kuhakikisha kuwa upanuzi wa mitaala, ufundishaji na tafiti zinazofanywa na chuo hicho zinaelekezwa katika kutoa michango na rai zitakazochangia na kurahisisha utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya nchi.
Akizungumza wakati wa mahafali ya tisa ya Chuo Kikuu hicho yaliyofanyika jana huko Tunguu, mara baada ya kuwatunuku vyeti, stashahada na shahada wahitimu 763, Dk. Shein amesema ni jukumu la vyuo vikuu hasa vya serikali kutoa taaluma inayolenga kurahisisha utekelezaji wa mipango ya maendeleo taifa na jamii kwa ujumla.
Alisema zitihada zinazofanywa na chuo za kukuza elimu zitakuwa na manufaa zaidi endapo elimu itakayotolewa italiongoza Taifa na itatumika kurahisisha maisha na kuimarisha maendeleo kwa kusaidia utekelezaji wa Dira ya Maendeleo 2020, MKUZA II, Malengo ya Milenia na Ilani ya Uchaguzi ya CCM.
Dk. Shein aliwaeleza wahitimu, jumuiya ya wanachuo na wageni waliohudhuria mahafali hayo kuwa serikali inaziunga mkono jitihada zinazofanywa na chuo hicho za kuongeza mafunzo ya nyanja mbalimbali kwa kuwa inaamini kuwa maendeleo ya nchi yanategemea nguvukazi yenye elimu ya kutosha.
Alisisitiza kuwa serikali ina kila sababu ya kuimarisha maslahi ya watumishi wa SUZA kila hali ya uchumi itakaporuhusu na kuongeza kuwa azma ni kuhakikisha kuwa maslahi yanakuwa mazuri hadi kuwavutia wale walioko nje kurudi chuoni hapo.
Alisema ameridhika na jitihada za chuo hicho za kuzidi kuongeza nyanja za masomo ambapo katika kipindi kifupi chuo hicho kimeweza kuongeza programu mpya tisa zikiwemo mbili za shahada za uzamili, fani tano za kiwango cha shahada na mbili za kiwango cha stashahada.
Alikipongeza chuo kwa kuanzisha mafunzo ya shughuli za ujasiriamali na ubunifu hatua ambayo aliieleza kuwa itasaidia jitihada za serikali za kuwawezesha wananchi kiuchumi.
Wakati huo huo Makamu Mkuu wa SUZA Profesa Idris Ahmada Rai, alisema kuwa katika kuimarisha uwezo, chuo kimeweza kufanikiwa kupata rasilimali mbalimbali kupitia utaratibu wa ushindani kwa wanataaluma wa chuo hicho kupeleka miradi na tafiti zao.

No comments :

Post a Comment