Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, December 23, 2013

Dk. Shein: Zanzibar wenyewe ni Waafrika

A4087

RAIS wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, amesema Zanzibar ni nchi iliyo katika bara la Afrika ambayo ilipaswa kujikomboa na kuwa huru ili kujitawala wenyewe na si kuendelea kubaki chini ya utawala wa kikoloni.

Dk. Shein alisema hayo jana katika uwanja wa mpira wa Shule ya Msingi Micheweni, Mkoa wa Kaskazini Pemba, wakati akizindua matembezi ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) katika maadhimisho ya miaka 50 ya mapinduzi ya Zanzibar.
Alisema mapinduzi ya Zanzibar yalifanyika baada ya kushindikana kwa njia ya demokrasia katika chaguzi kuu zilizofanyika mara tatu kuanzia mwaka 1957, 1961 na 1963.
Alisema mara zote hizo chama cha Afro Shiraz (ASP) kilishinda uchaguzi, lakini wakoloni walikinyima madaraka ya utawala.
“Mapinduzi ya mwaka 1964 yalifanyika baada ya Waafrika kufanyiwa hila na mbinu chafu na wakoloni, baada ya kukwamishwa wazee wetu walitumia ujasiri na kumwaga damu ili kuleta ukombozi na uhuru kamili,” alisema.
Dk. Shein ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, aliwataka vijana katika kizazi kipya kuiga ujasiri, uzalendo na ukweli wa wazee hao na kukitaja kitendo hicho kuwa hakitasahaulika katika historia ya Zanzibar.
Aidha, aliwataja wana mapinduzi ya Zanzibar chini ya uongozi wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar hayati Mzee Abeid Amani Karume kwamba wao na wanachama wao walikuwa na mshikamano, mapatano na umoja wenye nguvu uliowasaidia kuwashinda wakoloni.
Walifikwa na majaribu mengi ya kutaka kugawanywa, walishikamana pamoja, hawakuyumba na hawakukubali kudanganyika ili waendelee kubaki chini ya utawala wa kigeni, wamepata ukombozi unaohitaji kulindwa,” alisema.
Awali, Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Zanzibar, Shaka Hamdu Shaka, alisema baada ya chama cha ASP kuchoshwa kutawaliwa, walijenga ushupavu na kuwa zaidi ya silaha zilizouondosha utawala wa kisultani.
Shaka alisema ujasiri wa wana mapinduzi ulikuwa ni zaidi ya silaha za moto zilizofanikisha mapinduzi ya umma na haki, hivyo UVCCM watahakikisha urithi huo unatunzwa na kuheshimiwa.
Chanzo Tanzania Daima

No comments :

Post a Comment