Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, December 26, 2013

Hoteli za kitalii Zanzibar kufungwa kamera za kiusalama

Na Mohammed Mhina


Jeshi la polisi Zanzibar limewaagiza wadau wa masuala ya utalii visiwani humo kuangalia uwezekano wa kufunga vifaa vya kiusalama, zikiwamo kamera za CCTV kwenye maeneo ya mahoteli na hata katika magari yanayotumiwa na watalii ili kusaidia kuwabaini wahalifu wanapofanya matukio ya kihalifu.

Agizo hilo lilitolewa na Kamishna wa Zanzibar, Hamdani Omari Makame, wakati akizungumza na viongozi wa Jumuiya za Wawekezaji wa Tasnia ya Utalii (Zati) na ile ya Waongoza Watalii Zanzibar (Zato) ofisini kwake, mjini Zanzibar.

Alisema kama maeneo ya mahoteli na yale yanayofanyiwa utalii yatafungwa kamera hizo, inawarahisisha polisi kuwatambua kwa urahisi wale wote wanaojihusisha na vitendo vya kihalifu katika maeneo hayo.
Alisema kutokana na kukua kwa teknolojia duniani, ni lazima wamiliki wa mahoteli nao kwenda sambamba na mabadiliko hayo ili kusaidia katika masuala ya kiusalama katika maeneo hayo.

Aidha, Kamishna Makame alisema tayari Jeshi la Polisi visiwani humo limeanzisha Kikosikazi kinachowashirikisha askari polisi, askari wa vikosi vya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) na wale wa utalii kwa lengo la kukabiliana na uhalifu katika fukwe za bahari zenye watalii wengi.

Awali, Mwenyekiti wa Zati, Abdul-Samad Saidi Ahmed, alisema jumuiya hizo zitaendeleza ushirikiano uliopo baina yao na Jeshi la Polisi kwa kusaidia vitendea kazi kwa jeshi hilo ili kumudu kukabiliana na uhalifu, ambao umekuwa kikwazo kwa sekta ya utalii visiwani humo.

Nao Naila Jidawi na Seif Masoud, ambaye ni Kamishna wa Utalii Zanzibar, walisema kuwa idadi ya ndege zinazoingiza watalii Zanzibar imepungua kutokana na kuzorota kwa hali ya usalama visiwani humo na kwamba suala la matukio ya tindikali ni moja ya sababu zilizochangia kudorora kwa uingiaji wa watalii.

Ujumbe huo ulifika ofisini kwa Kamishna Makame kwa lengo la kujitambulisha na kuelezea hali ya utalii na vikwazo vilivyopo sasa katika tasnia hiyo visiwani humo.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment