Lissu azungumzia maamuzi kuhusu Zitto
NA THOBIAS MWANAKATWE
24th December 2013
Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu, amesema chama hicho kitaendelea kusimamia misingi yake ya katiba na taratibu zake kwa ama kuwafukuza, kuwaonya au kuwasamehe viongozi na wanachama wanaopatikana na makosa ndani ya chama.
Aidha, amesema uamuzi wa kumvua nyadhifa zake Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, na wenzake wawili haujachukuliwa eti kwa sababu baadhi ya viongozi wandamizi wanachuki naye.
Lissu alisema hayo wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Sherui Jimbo la Iramba Magharibi mkoa wa Singida katika mkutano wa hadhara.
Aidha, amesema uamuzi wa kumvua nyadhifa zake Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, na wenzake wawili haujachukuliwa eti kwa sababu baadhi ya viongozi wandamizi wanachuki naye.
Lissu alisema hayo wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Sherui Jimbo la Iramba Magharibi mkoa wa Singida katika mkutano wa hadhara.
“Tulilazimika kufanya maamuzi magumu ya kuwavua nyadhifa akina Zitto ili kukijenga chama na tutaendelea kufanya maamuzi zaidi na ikibidi kufukuza, kukemea na kusamehe bila kumuonea mtu wala kumpendelea,” alisema.
Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki, alisema chama chochote cha siasa ni lazima kifuate desturi na katiba yake kwani bila kufanya hivyo wananchi watakosa imani nacho.
Alisema nafasi ya Naibu Katibu Mkuu aliyokuwa nayo Zitto kabla ya uamuzi wa Kamati Kuu ni ya nne, lakini inashangaza inafikia kiongozi anamwita Mwenyekiti wa Taifa wa chama ana akili ndogo tena kwa maandishi na kuyaweka kwenye mitandao ya kijamii.
Lissu alijoji je, Zitto kama angekuwa CCM akamwita Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho kwamba ana akili ndogo je, angepona?”
Alisema chama chochote cha siasa kiwe ni CCM, CUF au Chadema kina sheria na katiba zake na kwamba mtu anayefikilia kuwa Zitto alichukuliwa hatua hizo kutokana na labda Dk. Slaa, Lissu na Mbowe wanachuki naye ni hoja dhaifa na ya uongo.
Alisema mwaka 2007 Zitto alipofukuzwa Bungeni baada ya kuzungumzia suala la mgodi wa Buzwagi yeye (Lissu) na Dk. Slaa ndiyo waliomtetea na kwenda jimboni kwake kijiji cha Mwandiga na kuwaeleza kuwa alichokisema ni sahihi hivyo alionewa.
Alisema maamuzi yaliyochukuliwa na yanapaswa kupongezwa kwa sababu hata chama tawala kinaogopa kuyafanya.
CHANZO: NIPASHE
No comments :
Post a Comment