NA LULU GEORGE
18th December 2013
Nishati hizo zimebainika kuwapo katika wilaya za Tanga, Pangani na Mkinga na kwamba serikali kwa kushirikiana na watafiti hao wanaendelea na mchakato kufahamu kiasi kilichopo tayari kuanza kufanya majaribio ya rasilimali hiyo.
Akizungumza katika mahojiano na NIPASHE muda mfupi baada ya kufungua warsha ya wanahabari pamoja na asasi za kiraia kuhusu uzuruaji wa mafuta na gesi asilia iliyoandaliwa na Shirika la Kimataifa linalojihusisha na Hifadhi Mazingira (WWF), Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Halima Dendegu, alisema hatua hiyo ni mojawapo ya fursa za kiuchumi mkoani humu.
Dendego aliyataja maeneo ambayo hivi sasa yanafanyiwa utafiti na wataalam wa kimataifa kwa kutumia meli katika ukanda wa Bahari ya Hindi kuwa ni vijiji vya Marungu na Tongoni kwa upande wa Jiji la Tanga.
Akizungumzia hatua hiyo, Meneja Uhifadhi wa WWF, Gerad Kamwenda, alisema lengo hasa la kuwahusisha wanahabari katika mafunzo hayo ni kutokana na kutokuwa na usahihi wa habari zinazoandikwa kuhusu kuwapo kwa gesi na mafuta kwenye maeneo mbalimbali nchini na kwamba nyingi hazifanyiwi utafiti wa kina.
CHANZO: NIPASHE
No comments :
Post a Comment