Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, December 29, 2013

Mansour: Tusimame Pamoja Kuitetea Zanzibar

By Hamed Mazrui (Facebook Page)

WAZIRI wa zamani wa serikali ya Zanzibar, Mansour Yussuf Himid amesema Zanzibar ni ya Wazanzibari na ametaka wananchi kujielewa katika kusimamia hilo.
Amesema wananchi wanapaswa kujielewa kuwa Zanzibar ni mali yao wenyewe na hakuna ubia na watu wengine wasiyokuwa Wazanzibari.
Akizungumza leo Chaani, Mkoa wa Kaskazini Unguja kwenye mkutano wa hadhara wa Chama cha Wananchi (CUF) Mansour, alisisitiza kwa Wazanzibari kutokurudi nyuma katika kutetea Zanzibar, yenye MAMLAKA kamili:
“Napenda kusisitiza kwenu wananchi kutokukubali kurudi nyuma katika suala zima la kuitetea Zanzibar…bila ubaguzi wa aina yoyote,” alisema Masour.
Mansour ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Maridhiano, katika mkutano huo alialikwa kama mjumbe wa Kamati hiyo, ambapo alisema wakati Mzee Karume ametuhakikishia urithi wa Nchi hii basi kila mmoja wetu ana haki sawa na mwengine.
Alitaka Wananchi hususan vijana kutokukubali kurudi tena nyuma kwa sasa katika suala zima la kuitetea Zanzibar,  yenye MAMLAKA kamili.
Alisema wananchi wa Zanzibar ni waungwana sana lakini vile vile si wajinga, wanapodai haki yao, hakuna sababu ya kudharauliwa: “Tusilazimishane tunapokataa mfumo wa Muungano wa serikali mbili,” alisema Mansour.
Aidha, alisema anawashangaa sana baadhi ya viongozi wanaotoa kauli za kuwatisha wananchi wanaotaka Zanzibar, yenye MAMLAKA kamili.
Mansour ambaye alifukuzwa uanachama wa CCM miezi michache iliyopita, alimsifu Maalim Seif Sharif Hamad, huku akisema hajawahi kumsikia kutoa lugha ya matusi si kwa wananchi wala kwa viongozi.
‘’Binafsi sijawahi kumsikia Maalim Seif akikemea wananchi juu ya maamuzi yao wanayotaka…Iweje leo wengine watumie nafasi za uongozi kuwatisha wananchi?,’’alihoji Mansour.
Naye, Mwenyekiti wa Kamati ya Maridhiano, Hassan Nassor Moyo alisema madai ya sasa ya Wazanzibari, si mambo mageni kwa sababu yalikuwapo kabla ya kuja kwa Muungano:
“Tunayodai sasa kwa nchi yetu si mageni yote tulikuwa nayo hapo awali kabla ya Muungano,” alisema Mzee Moyo.

No comments :

Post a Comment