Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, December 22, 2013

Mbeya Cement yanzindua mashine ya kunyonya vumbi

NA MWANDISHI WETU

16th December 2013


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Maria Bilia, akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa mashine maalum ya kunyonya vumbi katika kiwanda cha kuzalisha saruji cha Mbeya Cement Lafarge Tanzania. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Biashara katika wizara hiyo na pia Mjumbe wa Bodi wa Kampuni ya Mbeya Cement, Deodatus Ndunguru.
Kampuni ya Saruji ya Mbeya Cement Lafarge Tanzania, jana ilizindua mashine ya kisasa ya kunyonya vumbi.

Mashine hiyo itapunguza vumbi linalotoka wakati wa uzalishaji hadi kufikia 10mg/nm3 kiasi ambacho ni kidogo kuliko kiwango kilichowekwa na taasisi ya kanuni za mazingira nchini cha 50mg/nm3.

Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa mashine hiyo iliyofanyika kwenye kiwanda hicho kilichopo Songwe jijini Mbeya, Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Catherine Langrency, alisema mradi huo umegharimu Euro milioni 1.5 (sawa na Shilingi bilioni tatu).

"Uzinduzi wa mashine hii unadhihirisha nia thabiti ya Mbeya Cement ya kuendelea kuboresha shughuli za uzalishaji ili kukidhi matakwa ya kampuni mama ya Lafarge ya kufanya shughuli za uzalishaji bila kuathiri mazingira ifikapo 2020," alisema Langrency.

Langrency alisema Lafarge imeamua kutumia tekinolojia ya mashine ya kuchuja vumbi ili kuhakikisha kwamba mfumo wa kazi hiyo hauathiriwi na kukatikakatika kwa umeme.

"Tunafanya kazi kwa kushirikiana na Balaza la Taifa la Hifadhi ya Mazingira (Nemc), jamii inayotuzunguka, na wadau wengine kuboresha hali ya mazingira na kuwa mfano bora miongoni mwa viwanda vya saruji nchini Tanzania," alisema.

Hafla hiyo ya uzinduzi iliongozwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Maria Bilia, kwa niaba ya Waziri wa wizara hiyo, Dk. Abdallah Kigoda.

Aliipongeza kampuni ya Mbeya Cement Lafarge Tanzania kwa kuonyesha njia na kutoa wito kwa Watanzania kuwaunga mkono kwa kununua na kutumia saruji inayozalishwa hapa nchini.

"Kwa kufanya hivyo, tutawawezesha kuzalisha zaidi hivyo kupanua wigo wa ajira kwa vijana wetu,"   alisema.

Langrency pia alisema kampuni yake iko mbioni kuongeza uwezo wake wa uzalishaji hadi kufikia tani 700,000 kwa mwaka kwa kuweka mashine nyingine mpya ya kuzalisha saruji na mpango mwingine mpya wa kufungashia.

Mradi huu unatarajia kukamilika ndani ya robo ya pili ya mwaka 2015, ikiwa ni awamu ya kwanza ya upanuzi mkubwa wa Mbeya Cement nchini Tanzania.

“Upanuzi huu utaongeza maradufu uzalishaji wetu wa saruji na kutuwezesha kukidhi mahitaji ya saruji," alisisitiza.
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment