zanglassworks

AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, December 4, 2013

Msiogope kukopa fedha benki,JK awaambia wananchi

NA JUMA NG'OKO

4th December 2013


Rais Jakaya Kikwete
Rais Jakaya  Kikwete amewataka wananchi wasiogope kukopa fedha katika taasisi za fedha na benki nchini kwa ajili ya kuanzisha miradi na kujiletea maendeleo .

 Kikwete alitoa rai hiyo juzi wakati akizindua Tawi la  Benki  ya Azania Limited katika Kijiji cha  Lamadi kilichopo Wilaya ya Busega  mkoani Simiyu mapema wiki hii.

" Fedha haziokotwi barabarani, na wala huwezi  ukanyeshewa  na fedha kama mvua.

Fedha  za uhakika  kwa ajili  ya biashara  endelevu  hutokana  na mikopo  katika taasisi  za kifedha," alisema     Kikwete  huku  akiwaasa  wananchi  wasiogope  kukopa ili mradi  wazingatie  kurejesha mikopo  hiyo  kwa wakati.

Alisema fedha  ni kichocheo  muhimu sana  cha  maendeleo  ya kila  binadamu  na kwamba Serikali  yake  itaendelea  kushirikiana  na taasisi  za fedha, ikiwamo  benki  hiyo kuhakikisha uchumi  wa mtu mmoja mmoja, kaya  hadi taifa  unakuwa kwa kasi  kadri  inavyowezekana

Aliwataka  wakazi  wa kijiji  hicho na vya jirani    kufungua akaunti katika benki  hiyo  na kuomba  mikopo itakayowasaidia kuanzisha miradi ya biashara na kuwa na maisha bora.

" Ninawapongeza  sana Azania Benki  kwa  kutambua  umuhimu  wa kuwekeza huduma  za kibenki, hasa  maeneo  ya vijijini, "  alisema na kuongeza kuwa  hatua hiyo itawavutia  wawekezaji  wengi  zaidi  katika  maeneo  ya vijijini na kasi ya wananchi kujiletea maendeleo.

Awali Mkurugenzi  Mtendaji  wa Benki hiyo, Charles  Singili,  alisema ufunguzi   wa tawi hilo  katika  kijiji  hicho ni sehemu  ya  kutekeleza  agizo lililotolewa  na Rais Kikwete wakati  akifungua tawi  lao Mwaloni-Kirumba  jijini Mwanza mwaka 2006.
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment