NA BEATRICE SHAYO
22nd December 2013
Aliyasema hayo jana katika hafla ya kukabidhi vifaa vya muziki kwa vijana wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) vyenye thamani ya Sh milioni 13 .7 kwa ajili ya shughuli za maendeleo.
Alisema vyama vya TANU na ASP vilifahamu thamani na umuhimu wa kuitumia nguvu kazi ya vijana na kaumua kuwajenga kiakili, kiitikadi na kisiasa ili kupata vijana watiifu na waaminifu kwa taifa.
Alisema vyama vya TANU na ASP vilifahamu thamani na umuhimu wa kuitumia nguvu kazi ya vijana na kaumua kuwajenga kiakili, kiitikadi na kisiasa ili kupata vijana watiifu na waaminifu kwa taifa.
Alisema ni kazi inayotaka maamuzi ambayo humlazimu kila kiongozi kuhakikisha kuwa vijana wanathaminiwa, kuandaliwa kielemu na kutatuliwa kwa vitendo, changamoto zinazowakabili mahali popote.
Alisema kuwa Mapinduzi ya Zanzibar ya Januari 12 mwaka 1964 ndiyo yaliyoleta ukombozi wa kweli kwa wananchi wanyonge wa Unguja na Pemba ambao waliokosa fursa muhimu za kijamii.
Aliwataka vijana kutambua wajibu wao kwa taifa lao na kuwa tayari wakati wote kufanya kazi kwa bidii, maarifa na kukataa kujiingiza katika mambo yanayioweza kuwavunjia hadhi zao.
Alisema kuwa vijana wanatakiwa kujiwekea mikakati yao ya kujitafutia ajira na sio kujiingiza kwenye matendo maovu kwani kutasababishia kukosekana kwa nguvu kazi ya vijana.
Kwa upande wake Mke wa Makamu wa Pili wa Rais Mama Asha Suleiman Idd alitoa wito vijana na kuwataka kukataa kudanganyika na badala yake waendelee kuziiamini sera za CCM.
Mama Asha alisema bila ya CCM yenye viongozi wazoefu wa kusimamia uendeshaji nchi unaofuata na kuheshimu misingi ya utawala bora wa ksheria, Tanzanai inaweza kujikuta ikiyumba.
Aliwaeleza wananchi kuwa huwa anafurahishwa kufanya kazi na Mama Mwanamwema na kumtaja kuwa amekuwa mtu wa karibu kwake wakati wowote katika kushughulikia matatizo ya maendelo ya jamii na kwamba wataendelea kuwa pamoja katika kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili vijana.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Zanzibar, Shaka Hamdu Shaka, alitoa pongezi kwa wake hao wa viongozi wa Zanzibar na kusema wamekuwa washauri na viungo kati ya CCM na jumuiya zake tatu yaani vijana, wazazi na wanawake kwa kutoa mawazo pamoja na kuwashauri.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
No comments :
Post a Comment