Waziri Mstaafu wa Ulinzi na Jeshi la kujenga taifa, Mhe Shamsi Vuai Nahodha alipokuwa akizungumza na WanaCCM kwenye jengo la Makao Makuu ya CCM Mkoa wa Mjini Magharibi Amani jana.
Mwakilishi wa jimbo la Mwanakwerekwe Shamsi Vuai Nahodha amesena anaungana na kundi la wazanzibar wanaotaka Zanzibar kuwa na mamlaka kamili ndani ya katiba ijayo ya jamhuri ya muungano Tanzania.
Akizungumza na wanachama na viongozi katika ofisi za CCM mkoa wa mjini kichama amesema katika baadhi ya maeneo ya kuendesha nchi suala la mamlaka kamili ni muhimu kuimarisha uchumi wa Zanzibar.Nahodha aliewahi kuwa waziri wa mambo ya ndani na waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa amedai yeye ni mtetezi wa suala la mafuta na gesi liondolewe kwenye muungano.
Hata hivyo amesema anashangazwa na baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa wanaodai sarafu ya Zanzibar, kiti cha umoja wa mataifa na wizara ya ulinzi akidai masuala hayo yanahitaji gharama kubwa za uendeshaji.
Aidha Nahodha amesema wakati Zanzibar ikiendelea kuadhimisha miaka 50 ya Mapinduziu Zanzibar muungano utaendelea kubaki uti wa mgongo wa maendeleo ya ulinzi na usalama wake.
Amesema licha ya mfumbo wa muungano wa serikali mbili kujaa matatizo, lakini njia ya kuyapatia ufumbuzi ziko huru badala ya kun'gan'gania muungano wa mkataba au serikali tatu akidai haiku salama na Zanzibar
Chanzo: Zanzibar Islamic News Blog
No comments :
Post a Comment