dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, December 25, 2013

Shein ajivunia mafanikio miaka 50 ya Mapinduzi

NA MWANDISHI WETU

25th December 2013


Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein
Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein,  amesema miaka 50 ya Mapinduzi, Zanzibar imeshuhudia mabadiliko makubwa katika sekta ya elimu.
Rais Dk. Shein amesema wakati huu Zanzibar ikiadhimisha miaka 50 ya Mapinduzi, wananchi hawana budi kujivunia maendeleo makubwa yaliyopatikana katika sekta hiyo ya elimu.
Aliyasema hayo katika sherehe za ufunguzi wa Skuli ya Sekondari Chasasa na Skuli ya Sekondari ya Wanawake ya Utaani Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Hiyo ilikuwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi ya mwaka 1964.
Alisema vikwazo vya elimu kabla ya Mapinduzi haikuwa ada ya skuli pekee, lakini hata fursa zenyewe hazikuwapo kwa watoto wa familia maskini kwani mtu angeweza kupata ada lakini akashindwa kupata nafasi kwa kuwa anatoka familia ya kinyonge.
 Alisema madhila ya aina hiyo waliyokuwa wakifanyiwa wananchi maskini wa Zanzibar, ndiyo yaliyokifanya Chama cha Afro Shirazi kusimama kidete kutetea haki za wanyonge.
Alisema azma ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar tangu wakati huo ni kuwapatia elimu watoto wote hadi kikomo cha uwezo wao na ndiyo maana kila wakati imekuwa ikiongeza fursa za elimu nchini.
CHANZO: NIPASHE

1 comment :

  1. Alau serikali ya SMZ ingejenga shule moja tu yenye hadhi kama ya Haileselsie katika kipindi hicho cha nusu karne
    lakini tunawaona watoto wetu wakitoka vibyongo kwa kukaa chini na kuinama muda mrefu. Pengine Shein hakuyapata kwa watoto wake ambao walizaliwa Uingereza. Kujipongeza huko ni kutukebehi

    Watoto wetu waliowengi wanatumia vibatari kama njia ya nishati kujisomea. wazee hawawezi kulipia gharama kubwa za umeme.

    Leo mtoto mwenye shahada hawezi kulinganishwa na mtu wa darasa la nane aliehitimu n a bila ya kujiendeleza. mfano hai mwenye shahda wa matunda ya mapinduzi hafui dafu kwa Mhe. Abdulla Mwinyi mwenye darasa la nane la ukoloni

    hivi ni haki kujivunia hali hii?

    ReplyDelete