Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, December 27, 2013

'Wazanzibar msibaguane kwa dini, siasa na ukabila'

NA RAHMA SULEIMAN

27th December 2013


Mbunge wa jimbo la Mtera, Livingstone Lusinde
Mbunge wa jimbo la Mtera, Livingstone Lusinde, amewataka Wazanzibar kuacha kubaguana kwa misingi ya dini, siasa na ukabila.

Akizungumza jana katika mkutano wa hadhara wa CCM katika jimbo la Mpendae, alisema kuna baadhi ya watu visiwani hapa wanahubiri dini kwa misingi ya chuki ili kuwagawa Wazanzibar.

Alisema si vyema kubaguana kwa ajili misingi ya dini, siasa wala ukabila na badala yake kuhubiri amani na usalama wa nchi.

Aliwataka wanasiasa wanapokaa majukwaani kuacha kuwakashifu viongozi wa nchi kwani mafanikio yaliyopatikana hapa nchini yanatokana na viongozi wa nchi hiyo.

Sambamba na hayo aliwataka wanachama wa chama cha mapinduzi kuzidi kushiriana ili kuweza kukiletea ushindi chama hicho ifikapo mwaka 2015 katika uchaguzi mkuu.

Mwakilishi na Mbunge wa jimbo hilo, Muhammed Said na Salum Turkey walisema watahakikisha wanatekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi ili kuweza kuliletea maendeleo jimbo hilo.

Walisema kwa kipindi cha miaka mitatu wameshatumia zaidi ya milioni 50 kwa kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika jimbo hilo. 
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment