NA JIMMY MFURU
16th December 2013
Ripoti ya Benki ya Dunia (WB) ilisema kama ilivyokuwa miaka ya hivi karibuni, kukua kwa uchumi wa Tanzania kunaonekana kusukumwa na sekta, ambazo shughuli zake sehemu kubwa ziko katika miji, katika sekta za mawasiliano, uchukuzi, ujenzi na biashara za rejareja.
Ripoti hiyo inajenga hoja ya kuongeza uzalishaji katika kilimo na kutengeneza ajira nyingi nje ya shughuli za kilimo.
Inasisitiza kuwa mikakati kama hiyo haitoshi kumfanya kila mtu aondoke kwenye umaskini wakati uzoefu duniani unaonyesha hata kama uzalishaji katika kilimo utaongezeka, huku familia maskini zaidi kawaida zikiachwa nyuma.
“Hii inaonyesha umuhimu wa kuwa na programu za hifadhi ya jamii zinazolenga kuwasaidia watu walio katika mazingira hatarishi zaidi,” alisema Mkurugenzi wa WB Tanzania, Uganda na Burundi, Philippe Dongier.
Ripoti ya hivi karibuni ya Hali ya Uchumi inaonyesha mafanikio ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf).
Inaonyesha matokeo mazuri katika kushughulikia mahitaji ya kaya maskini zaidi, wazazi wanaopata kiasi kidogo cha fedha kila mwezi hutumia fedha hizo kununua chakula cha ziada na mahitaji ya elimu na afya ya watoto wao.
CHANZO: NIPASHE
No comments :
Post a Comment