Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, December 20, 2013

ZANZIBAR: HABARi MCHANGANYIKO

  • Darajani hakikuwa kituo cha Daladala
  • WANAFUNZI WA ZANZIBAR WAHAMASISHWA KUSOMEA FANI YA MAFUTA
  • MADAKTARI HAWATAKI KUFANYA KAZI PEMBA

Kilichokua kituo cha magari ya abiria, Darajani
Kilichokua kituo cha magari ya abiria, Darajani Zanzibar
ZANZIBAR: SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema imechukua uzoefu wa kuondosha vituo vya daladala katika Jijini Dar es Salaam na baadhi ya nchi za Afrika Mashariki. Waziri wa Nchi, Afisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Idara Maalumu za Serikali, Haji Omar Kheir ameyasema hayo jana katika kikao cha baraza la wawakilishi kilichoendelea mjini Zanzibar.
Akijibu suali la msingi la Mwakilishi wa Jimbo la Muyuni (CCM) Jaku Hashim Ayoub aliyetaka kujua Baraza la Manispaa la Zanzibar limechukua uzoefu kutoka nchi gani za Afrika Mashariki katika kupanga vituo vya daladala ambavyo vimekuwa ni usumbufu mkubwa kwa wananchi hivi sasa tokea kuhamishia kituo kikuu cha Darajani.
Kheri alisema baraza la manispaa katika kutekeleza suala la kuhamisha vituo vya daladala limeanza kwa kuangalia uzoefu wa zamani uliokuwa uikitumika hapo Zanzibar ambapo kituo kikuu cha daladala hakikuwepo eneo la Darajani.Alisema uzoefu waliochukua Zanzibar katika nchi za Afrika Mashariki ni Dar es Salaam ambapo waliondosha kituo chao cha daladala na kukihamishia sehemu nyengine ya jiji ili kuondosha msongamano wa magari na uchafuzi wa mazingira.
Alisema eneo la Darajani penye kituo kilichofungwa kwa sasa ni eneo la wazi kwa matumizi ya wananchi na serikali kupitia baraza la manispaa ambapo lilitangaza eneo hilo katika mpango wa uendelezaji wa eneo zima la Darajani.
Alisema serikali haijakataza magari ya abiria kushusha na kuchukuwa abiria katika maeneo ya mjini na Darajani.
Akijibu suali la nyongeza la Mwakilishi wa jimbo la Chonga, Juma Abadalla Juma (CUF) Kheir alisema kuwa Serikali ilichokifanya ni kuondosha kituo cha daladala katika eneo la Darajani na si kukataza wasishushe au kuchukuwa abiria.
 
Watu wasichanganye mambo na wawakilishi wawaeleze wananchi kilichofanyika hapo, tukianza kusema na kupinga kila kitu japo jambo lina faida kwa wananchi tutakuwa hatuwatendei haki wananchi”, alisema Kheri.
 
Waziri huyo alisema kuwa serikali imeamuwa kuchukuwa maamuzi hayo ikiwa tayari kukamilisha mpango wake wa kulitengeneza eneo hilo ili kuuweka mji mkongwe katika mazingira bora.
 
Akijibu suali la baada ya kufungwa eneo la Darajani , Serikali ina mpango gani wa baadae na eneo hilo au tayari amepewa mwekezaji, Kheri alisema serikali haijampa mwekezaji yeyote eneo hilo isipokuwa ni katika kupanga mipango miji.
Aidha alisema eneo la Michenzani limepangiwa matumizi maalumu na halitaweza kuwa kituo cha daladala na hivyo ushauri wa wajumbe kutaka eneo la Michenzani ndio liwe kituo kikuu cha daladala haitawezekana.
********************************************************************************************************
WANAFUNZI WA ZANZIBAR WAHAMASISHWA KUSOMEA FANI YA MAFUTA
WIZARA ya Ardhi, Maji, Nishati na Ardhi imesema kuwa imeandaa utaratibu maalumu wa kuwahakikishia kupata mikopo wanafunzi ambao wana sifa za kuendelea na mafunzo ya mafuta na gesi ikiwa pamoja na kuwahamasisha wanafunzi wa kidato cha sita kusomea fani hiyo.
 
Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Haji Makame Mwadini alisema ndani ya baraza la wawakilishi kwamba utaratibu huo unafanywa kwa mashirikiano ya karibu kati ya wizara hiyo na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali.
 
Alisema kuwa utaratibu huo pia utahusisha na mambo  yote ambayo yanahusiana na masomo hayo kwa wale ambao wamepasi masomo yanayolinga na somo hilo.
Alisema Serikali bado inaendelea na kushirikiana na washirika wa maendeleo wengi zaidi na kuwataka wawasaidie katika kuwasomesha wanafunzi wa Zanzibar katika fani hiyo ili kuja kufanya kazi ya mafuta.
Mwakilishi wa jimbo la Kwamtipura (CCM) Hamza Hassan Juma alitaka kujuwa Serikali ina mpango gani madhubuti na wa muda mrefu wa kuwasomesha wazanzibarI katika sekta ya mafuta ili uzalishaji utakapoanza malalamiko ya kuchukuliwa ajira na wasiokuwa wazanzibari yasije kujirudia katika sekta hiyo.
Katika suali lake la msingi Juma alitaka pia kujua ni wanafunzi wangapi ambao tayari wameshapatiwa mafunzo na serikali ya Ras el Heima ambapo katika bajeti ya mwaka juzi serikali ilihidi kusomeshewa wanafunzi wa Zanzibar katika fani hiyo.
Waziri alisema jumla ya wanafunzi kumi ndio walioahidiwa kusomeshwa na serikali hiyo ambapo tayari wanafunzi watatu wameshapelekwa masomoni na waliobaki watapatiwa mafunzo hayo mwakani.
 *************************************************************************************************
MADAKTARI HAWATAKI KUFANYA KAZI PEMBA
ZANZIBAR: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imesema jumla ya Madaktari 36 kati ya 162 wamekimbia kufanya kazi katika vituo vya Pemba mwaka 2011.
 
Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Afya Dkt. Sira Ubwa Mamboya alipokuwa akijibu suali la mwakilishi wa viti maalumu,Mwanaidi Kassim (CCM) katika kikao cha baraza hilo kilichoendelea visiwani Zanzibar.
 
Alisema kuwa kitendo hicho kinafanywa na madaktari wazawa wa kisiwa hicho ambao baadae hurudi katika kisiwa cha Unguja kufanyakazi kwa sababu wanazozijuwa wenyewe.
 
Na wengi wao hao ni wanaotoka Pemba, na ilibidi wale wachache wanaotoka Unguja waendelee kubakia kwani kama wangaliondoka ingalibidi hospitali zifungwe”, alisema.
 
Hata hivyo alisema kuwa kitendo hicho kinachofanywa na madakatari hao wazawa kinawafanya na madaktari wazawa wa Unguja kukataa kwenda kufanya kazi.
 
Wahitimu kutoka Pemba kukataa kurudi kufanya kazi Pemba wakipangiwa kwa visingizio mbali mbali ukiwapeleka wanakimbia na kuacha kazi jambo ambalo linawafanya na wale wa waunguja wanapopangiwa kukataa”, alisema.
 
katika suali lake Mwanaidi alitaka kujuwa sababu zilizopelekea upungufu wa madaktari wakati kila mwaka Chuo Cha Sayansi ya Afya na vyuo vyengine vya nje ya Zanzibar navyo vinasomesha wanafunzi kutoka Zanzibar.
Dkt Sira alisema kwa mujibu wa takwimu ya idadi ya rasilimali watu wa kada za afya kuna upungufu kote katika visiwa vya Unguja na Pemba lakini kwa kiwango kikubwa ni kutoka Pemba.
Akieleza sababu kubwa za wafanyakazi hao kukimbia Dk Sira alisema wafanyakazi wa afya kabla ya kuajiriwa wanafunga mkataba na kupa kwamba watafanya kazi popote Zanzibar.
Lakini wakishaajiriwa tu basi yale masharti ya ndnai ya mkataba wao huwa hayafuatwi tena hasa wakiwa na mahusiano au na ujamaa na wakubwa basi ndio kabisa wanachagua wao sehemu za kufanya kazi badala ya kupangiwa na wizara” alisema Naibu Waziri huyo.

Chanzo: ZanzibariYetu

No comments :

Post a Comment