Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, December 15, 2013

Ziara ya waandishi wa Habari kuangalia miradi ya maendeleo Pemba

MENEJA wa kiwanda cha Mafuta ya Makonyo Wawi 
Chake Chake Pemba, Ramadhan Kombo Feruzi akizungumza 
na ujumbe wa waandishi wa habari kutoka tanzania bara 
ba Zanzibar, wakati walipofanya zaiara yao ya kuangalia 
miradi mbali mbali ya maendeleo katika kiwanda hicho.
(Picha na Abdi Suleiman, Pemba.)

MKUU wa ghala la makonyo lililomo ndani ya kiwanda 
cha makonyo wawi Chake Chake Pemba, Hamad Said Omar, 
akiwaonyesha waandishi wa habari kutoka vyombo mbali 
mbali vya habari Tanzania bara na Zanzibar, makonyo 
gredi ya kwanza. 
(Picha na Abdi Suleiman, Pemba.)

INJINIA wa mtambao wa kisasa wa kuangalia ubora wa 
mafuta ya Mimea uliomo ndani ya kiwanda cha Makonyo 
wawi Pemba, Anton Pretorius akitoa maalezo kwa waandishi 
wa habari kutoka vyombo mbali mbali vya habari Tanzania 
bara na Zanzibar walipotembelea kiwanda hicho.
(Picha na Abdi Suleiman, Pemba.)
MSAIDIZI meneja wa kiwanda cha Makonyo wawi 
Chake Chake Pemba, Hamadi Ali Mohamed, akiwafahamisha 
waandishi wa habari kutoka Vyombo mbali mbali vya 
habari Tanzania bara na Zanzibar, juu ya mashine ya 
ufikichaji mafuta ya makonyo inavyofanya kazi wakati 
walipotembelea kiwanda hicho. 
(Picha na Abdi Suleiman, Pemba.)

MSAIDIZI meneja wa kiwanda cha Makonyo Wawi 
Chake Chake Pemba, Hamad Ali Mohamed, akiwafahamisha 
waandishi wa habari kutoka vyombo mbali mbali 
vya habari, kutoka tanzania bara na Zanzibar, 
juu ya mtambo wa kiwanda cha kukamulia mafuta 
ya makonyo unavyofanya kazi.
(Picha na Abdi Suleiman, Pemba.)


WAANDISHI wa habari kutoka vyombo vya habari 
Tanzania bara na Zanzibar, wakiangalia jiwe la 
msingi la kiwanda cha makonyo, lililowekwa na 
marehemu rais wa Mwalimu Julias Kambarage 
Nyerere mwaka 1982. 
(Picha na Abdi Suleiman, Pemba.)

MWANDISHI wa habari kutoka Habari Maelezo Pemba, 
Maruzuk Khamis akiangalia gredi ya kwanza ya 
makonyo safi, katika kituo cha ununuzi wa 
karafuu Mazambarauni Wilaya ya Wete, wakati wa 
ziara ya waandishi wa habari, kutoka vyombo vya 
habari Tanzania bara na Zanzibar. 
(Picha na Abdi Suleiman, Pemba.)

WAANDISHI wa habari kutoka Vyombo mbali mbali 
vya habari Tanzania bara na Zanzibar, wakizungumza 
na mkulima wa karafuu, katika kituo cha ununuzi 
wa zao hilo, mazambarauni Wete wakati wa 
ziara yao.
(Picha na Abdi Suleiman, Pemba.)

MKULIMA wa zao la karafuu katika kijiji cha 
Mtambwe akitandaza karafuu zake katika turubali, 
ili zikikauka kuziuza katika kituo kipya cah 
ZSTC Mtambwe, kilicho zinduliwa na Mhe dk 
Ali Mohamed Shein wakati alipofanya zaira 
yake kisiwani Pemba. 
(Picha na Abdi Suleiman, Pemba.)

MHANDISI mkaazi wa Wizara ya Miundombinu 
na Mawasiliano Pemba, Khamsi Mosuod Khamis 
akitoa ufafanuzi wa ujenzi wa barabara 5 za 
kisasa kwa kiwango cha lami, mkoa wa 
kaskazini Pemba.
(Picha na Abdi Suleiman, Pemba.)

GARI la kampuni ya H young likishindilia 
kokoto levuli ya mwisho katika barabara 
ya Kipangani hadi kangagani, ikiwa ni moja 
kati ya barabara tano za mkoa wa 
kaskazini Pemba. 
(Picha na Abdi Suleiman, Pemba.)

GARI maalumu la kampuni ya H young,
likitandaza kokoto baada ya kumwaga lami 
babarani,ikiwa ni hatua ya mwisho kukamilika 
kwa barabara, kama linavyoonekana katika picha. 
(Picha na Abdi Suleiman, Pemba.)

GARI la kubebea mizigo la kampuni ya 
H young likimimina kokoto katika gari maalumu 
ya kutandaza kokoto barabarani, katika barabara 
ya kipangani hadi kangagani, miongoni mwa barabara 
tano za mkoa wa kaskazi Pemba,kama linavyoonekana 
katika picha. 
(Picha na Abdi Suleiman, Pemba.)

Chanzo: ZanziNews

No comments :

Post a Comment