Jengo la Skuli mpya ya Ghorofa ya Mpendae lililofunguliwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ikiwa ni muendelezo wa shamra shamra za maadhimisho ya sherehe za mapinduzi ya Zanzibar kutimia miaka 50.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akikata utepe kuashiria kulifungua rasmi jengo jipya la skuli ya Ghorofa ya Sekondari ya Mpendae.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akikagua sehemu mbali mbali za skuli ya ghorofa ya Sekondari ya Mpendae mara baada ya kuifungua rasmi.
Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Sekondari ya Mpendae Mwalimu Mbarouk Rashid Habib akimpatia maelezo Balozi Seif mara baada ya kuifungua rasmi skuli hiyo.
“ Skuli sasa ipo nyumbani, kilichobaki ni juhudi yao tu ya kufanya vizuri katika masomo ya msingi ili waweze kuingia katika Skuli hii “. Alisema Balozi Seif.
“ Pamoja na masomo ya kawaida, ni muhimu pia kuwa na mafunzo ya ziada ambayo yatasaidia wanafunzi kuchemsha bongo ili kuondokana na kuwa na mambo yale yale (routine) kila siku darasani, ili waongeze motisha wa kusoma “. Alisisitiza Balozi Seif.
Katika risala yao walimu, wanafunzi na wazazi wa skuli ya Mpendae iliyosomwa na Mwalimu Muhaymina Talib Omar wameishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kushirikiana na washirika wa maendeleo katika jitihada za kukamilisha ujenzi wa Skuli hiyo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akikata utepe kuashiria kulifungua rasmi jengo jipya la skuli ya Ghorofa ya Sekondari ya Mpendae.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akikagua sehemu mbali mbali za skuli ya ghorofa ya Sekondari ya Mpendae mara baada ya kuifungua rasmi.
Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Sekondari ya Mpendae Mwalimu Mbarouk Rashid Habib akimpatia maelezo Balozi Seif mara baada ya kuifungua rasmi skuli hiyo.
Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
Na Othman Khamis Ame, OMPR
Skuli za Msingi na Sekondari zilizojengwa na zinazoendelea kujengwa katika sehemu mbali mbali za Visiwa vya Unguja na Pemba ni maeneo maalum yaliyotengwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuzalisha vijana wengi wa elimu ya juu watakaotegemewa kuwa chachu ya maendeleo ya Taifa hili.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo wakati akiifungua rasmi Skuli ya Sekondari ya Mpendae ikiwa ni muendelezo wa sherehe za Maadhimisho ya Kutimia miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964.
Balosi Seif alisema Wananchi wanaposherehekea miaka 50 ya Mapinduzi wanajinasibu kwa kuwa na Skuli za Sekondari 144 zenye jumla ya wanafunzi 76,706 ikiachiwa Chuo cha Ualimu cha Beit-el-Ras, ambacho kilichukua na idadi ndogo ya wanafunzi wa kusomea ualimu.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ameipongeza Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kwa kazi nzuri iliofanya katika kipindi cha miaka 50 takeo kufanyika kwa Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya mwaka 1964.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ameipongeza Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kwa kazi nzuri iliofanya katika kipindi cha miaka 50 takeo kufanyika kwa Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya mwaka 1964.
Balozi Seif alizitaja Miongoni mwa kazi hizo ni pamoja na kuendelea kuimarisha miundombinu ya elimu, kuipandisha hadhi sekta ya elimu hasa katika ujenzi wa skuli za msingi, sekondari pamoja na vyuo vya amali.
Aliwasihi vijana kutozichezea fursa zilizopo za kusoma na kuwataka kuongeza bidii ya ushindani ili wende sambamba na vijana wenzao wa Jumuiya ya nchi za Afrika Mashariki.
Alieleza kwamba kwa vile Serikali ina mpango wa kutoa kompyuta za kutosha kwa kila skuli ili wanafunzi waweze kutumia mitandao kwa ajili ya masomo yao aliwashauri kujifunza somo la kompyuta litakalowarahisishia kujifunza kwa urahisi zaidi.
Akizungumzia suala la kupanua kiwango cha taaluma Balozi Seif aliushauri Uongozi wa skuli ya Mpendae pamoja na masomo ya kawaida wakajipangia kuwa na mafunzo ya ziada ambayo yatasaidia wanafunzi kuchemsha bongo ili kuondokana na kuwa na mambo kila siku darasani.
Alieleza kwamba Skuli za sekondari zinaweza kuanzisha midahalo, michezo ya kuigiza kwa lugha ya Kiingereza na Kiswahili ili kurejesha mfumo ulokuwepo ambao ulisaidia kuimarisha kiwango cha elimu kilichoipatisa sifa kubwa Zanzibar wakati huo.
“ Mathalan, skuli za sekondari zinaweza kuanzisha “debating societies”, michezo ya kuigiza kwa lugha ya Kiingereza na Kiswahili. Mambo haya ambayo zamani yalikuwepo sasa hayapo tena. Ni vema kurudishwa katika skuli zetu za sekondari “ Aliendelea kufafanua Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.
Walisema ujenzi wa skuli hiyo umewapa faraja kubwa kutokana na uwepo wa huduma muhimu za lazima anazopaswa kuzipata mwanafunzi ikiwa ni pamoja na Maabara, Maktaba, Kompyuta pamoja na huduma za maji safi na salama.
Hata hivyo Walimu, Wanafunzi na Wazazi wa Skuli hiyo walizitaja baadhi ya changamoto zinazowasumbua ndani ya skuli hiyo ikiwemo ukosefu wa uzio wa skuli hiyo jambo ambalo linawapa wakati mgumu katika yulinzi wa skuli yao.
Mapema Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Bibi Mwanaidi Saleh alisema ujenzi wa skuli hiyo ya ghorofa ya sekondari Mpendae ni miongoni mwa skuli Mpya 19 za Sekondari zilizojengwa hapa Zanzibar.
Alisema skuli hizo zimo ndani ya mradi wa uimarishaji wa elimu ya lazima ambao unatekelezwa kwa pamoja kati yua Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kushirikiana na Benki ya Dunia { World Bank } kwa gharama ya Dola za Kimarekani Milioni 48.
Bibi Mwanaidi alisema uwepo wa skuli hiyo ya sekondari ya Mpedae utasaidia kupunguza msongamano wa wanafunzi uliopo katika skuli mbali mbali za jirani zilizopo Mwanakwerekwe.
Ujenzi wa skuli ya Mpendae ambao Mbunge wa Jimbo hilo Mh. Salum Turky na Mwakilishi wa Jimbo hilo Mh. Mohammed Said Mohammed Dimwa walioahidi kuweka mafeni kwenye madarasa yote ya skuli hiyo katika kipindi kifupi kijacho imegharimu zaidi ya shilingi za Kitanzania Bilioni 1.6.
Skuli hiyo yenye madarasa 12 ina uwezo wa kuhudumia wnafunzi wapatao 660 ambapo wanafunzi 40 kila darasa kwa mikondo miwili ikiwa kwa sasa ina wanafunzi sitini na moja.
Chanzo: ZanziNews
Chanzo: ZanziNews
No comments :
Post a Comment