NA RAHMA SULEIMAN
2nd January 2014
Alisema CCM inaimani na serikali mbili kutokana na serikali mbili ndiyo iliyoleta hali ya amani na usalama nchini. Akiwahutubia wanachama wa chama hicho katika mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya kwa mabata mjini hapa alisema kazi ya tume ya katiba imeshakwisha hivyo waamuzi wa mwisho wa mfumo huo uko mikononi mwa wananchi wenyewe baada ya kujadiliwa na wabunge wa bunge la katiba wanaotarajiwa kukamilisha kazi yao mwezi Febuari mwaka huu.
Alisema kazi kubwa iliyopo hivi sasa kwa wana CCM na wapenda amani nchini ni kuendelea kuimarisha muungano wa Tanzania ulioleta umoja na mshikamano na maelewano ya pande zote mbili.
Balozi Seif ambaye ni mlezi wa Mkoa wa Magharibi Kichama ambaye pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwahakikishia wana CCM hao kwamba Muungano wa Tanzania utaendelea kudumu . “ Wanachama wa Chama cha Mapinduzi msiwe na wasi wasi.
Muungano utaendelea kudumu na Aprili 26 mwaka 2014 unatimiza miaka 50 tangu kuasisiwa kwake “. Alisisitiza Balozi Seif.
Alisema Taifa limepata maendeleo makubwa tangu Zanzibar na Tanganyika zilipopata uhuru wake chini ya vyama vya TANU na ASP na baadaye Chama cha Mapinduzi yaliyoelekezwa kwa wananchi wote bila ya ubaguzi.
Alieleza kwamba upo ushahidi ulio wazi wa maendeleo hayo yaliyofanywa na Serikali zote mbili Nchini kwa kuwapelekea maendeleo wananachi wote ikiwa ni pamoja na huduma za maji, umeme, bara bara, mawasiliano na afya.
Alisema nguvu za chama cha Mapinduzi kupitia wanachama wake hivi sasa zielekezwe katika kuhakikisha chama hicho kinaendelea kushinda kwenye uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015.
CHANZO: NIPASHE
No comments :
Post a Comment