NA JIMMY MFURU
9th January 2014
Fedha hizo zitakazosaidia katika sekta binafsi, zimetolewa kupitia Taasisi ya Kimataifa ya Maendeleo ya benki hiyo (Ida), katika mkutano wa wakurugenzi hao uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana.
Kwa mujibu wa taarifa iliyosainiwa na Mkurugenzi Mkazi wa WB nchini Tanzania, Phillippe Dongier, na kusambazwa kwa vyombo vya habari na fedha hizo zinatakiwa zitumike kwa malengo yaliyokusudiwa ili kukuza uchumi wa Tanzania.
“Fedha hizo zimetolewa kwa lengo la kuimarisha mazingira bora ya biashara kwa sekta binafsi unaolenga hasa katika usimamizi bora wa ardhi,” ilifafanua taarifa hiyo ya Dongier.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Ida ilianzishwa mwaka 1960 kwa lengo la kusaidia nchi maskini kwa kutoa mikopo isiyokuwa na riba kwa lengo la kuendeleza masuala ya kukuza uchumi na kupunguza umaskini.
CHANZO: NIPASHE
No comments :
Post a Comment