Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, January 4, 2014

Hatimaye shule 'taabani' yakumbukwa

  • Mwantumu Mahiza, Abudul Muheji na wengine ni wakufukuzwa kazi immediately!!!
  • Hawana maana pesa mbili - ni mizigo tu kwa nchi!!!
  • Wakubwa wanashughulikia yao tu - hata kama pesa zipo wizarani hawajali kufuatilia!!!





NA MWANDISHI WETU
4th January 2014

Hatimaye Shule ya Msingi Machala ambayo iko taabani kutokana na jengo lake kuwa la nyasi tupu imekumbukwa na Serikali ya Mkoa wa Pwani baada ya kupewa  Shilingi milioni saba kati ya Sh. milioni 24 zilizotengwa kwa shule hiyo, matofali, saruji  na mabati.
Hatua ya kukumbukwa kwa shule hiyo inafuatia habari zilizochapishwa na gazeti hili wiki iliyopita ikionyesha hali halisi ya shule ambapo nyumba ya mwalimu na darasa vikiwa katika hali ya kusikitisha kutokana na kujengwa kwa udongo na nyasi.
Shule  hiyo ambayo pamoja na kuwa katika mazingira magumu na mwalimu mmoja tu, imeweza kufaulisha wanafunzi wote 12 katika mtihani wa darasa la saba, mwaka jana.Habari hiyo iliifanya Serikali Mkoa wa Pwani kuzinduka na kumlazimu Mkuu wa mkoa huo, Mwantumu Mahiza, kufanya ziara shuleni  hapo juzi na kutoa kiasi hicho cha fedha.
Fedha hizo ni kati ya Sh. milioni 24, zilizotengwa kwenye bajeti ya 2013/2014 kwa ajli ya ujenzi wa shule hiyo, lakini hazikuwahi kutolewa hadi juzi Mkuu wa mkoa alifanya ziara na kuwekwa kwenye akaunti ya shule.
Katika ziara hiyo Mahiza pia alitoa Shilingi milioni tatu na  ahadi ya matofali 1000 na mifuko ya saruji 100 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa na nyumba tatu za walimu.
Aidha, Mwalimu wa shule hiyo, Gelvas Rukutu, alizawadiwa pikipiki iliyosajiliwa ili iweze kumrahisishia katika shughuli zake kikazi na vitabu vya kiada vya kufundishia na vitabu vya wanafunzi  ambapo kila mwanafunzi atakuwa na kitabu chake. 
Akizungumza na wananchi, Mahiza aliwataka wananchi kujitolea kufyatua matofali ya kuchoma ili kuiondoa shule katika hali mbaya. 
“Wanannchi muwe tayari kujitolea nguvu zenu kuijenga shule  hii, hali hii siyo nzuri inaiaibisha serikali,” alisisitiza.
Aidha alimwagiza Afisa Elimu wa Mkoa huo, Abudul Muheji,  kupeleka walimu wawili  watakaoanza kazi mwezi huu  shule itakapofunguliwa, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wanafunzi wote wa kike waliofaulu wanapelekwa katika  shule za bweni ili waweze kusoma kwa raha na kuepuka mazingira magumu walioyazoea wakiwa shuleni hapo.
Akizungumza na NIPASHE Jumapili, mwishoni mwa wiki, Afisa Elimu Muheji alisema kuwa amewatangazia walimu wa shule za msingi zilizo jirani na kijiji cha Machala, watakaojitolea kwenda kufundisha  shule hiyo, watahakikishiwa stahili zao zote ikiwa ni pamoja na kupanda daraja, fedha za likizo usafiri na masuala mengine muhimu.
“Mimi nilichofanya baada ya kupewa agizo la kuwapeleka walimu nilitangaza bingo kwa walimu wa shule za msingi wilayani hapa wakikubali kwenda Machala watafurahi watafanikiwa katika huduma zote zinazostahili kwa mwalimu, tayari wamejitokeza walimu wawili,” alisema.
Akielezea chanzo cha shule hiyo kuwa katika hali hiyo mbaya, alisema  ni kutokana na kupangiwa bajeti ya ujenzi tangu mwaka 2007 ambazo ni Sh. milioni 25 lakini haikupata fedha hizo hadi bajeti ya 2013/2014 iliyopangwa Sh. milioni 24 na kati ya hizo kupewa Sh. milioni 7 tu ambazo zilitolewa juzi baada ya Mkuu wa mkoa kufanya ziara shuleni hapo.
Naye Mwalimu  Rukutu,  alilishukuru gazeti la NIPASHE Jumamosi kwa kuchapisha habari hiyo na uongozi wa mkoa  na ujumbe wake huku akitokwa na machozi kwa kuikumbuka shule hiyo ambayo ilisahaulika na serikali.
Alisema hii ni mara ya kwanza kwa shule hiyo kutembelewa na viongozi tangu ilipoanzishwa mwaka 2007.
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment