Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, January 17, 2014

Viongozi wakuu wamuaga Liundi

NA JIMMY MFURU

17th January 2014.

Rais Jakaya Kikwete na viongozi wengine wakitoa heshima za mwisho mbele ya mwili wa aliyekuwa Msajili wa Vyama vya Siasa mstaafu, George Liundi, kwenye viwanja vya Karimjee Dsm jana.
Vigogo wa serikali na vyama vya siasa jana waliungana na wakazi wa Jiji la Dar es Salaam kuaga mwili wa aliyekuwa Msajili wa kwanza wa Vyama vya Siasa nchini, George Liundi, aliyezikwa jana katika makaburi ya Chang’ombe.

Wakazi hao waliongozwa na Rais Jakaya Kikwete katika viwanja vya Karimjee wakiwamo viongozi mbalimbali.

Wengine ni Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal; Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa; Makamu wa kwanza wa Rais ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad; Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Warioba; Msajili mstaafu wa vyama vya Siasa, John Tendwa; Mwenyekiti wa NCCR- Mageuzi, James Mbatia na viongozi wengine waandamizi wa serikali na vyama vya siasa.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi, alisema Liundi atakumbukwa kwa kuwa alikuwa na mchango mkubwa katika ofisi ya msajili wa vyama vya siasa na kuwa alikuwa msajili wa kwanza katika mfumo wa vyama vingi.

Aidha, Lukuvi alisema Liundi alikuwa mwandishi mkuu wa sheria wa kwanza katika ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na alikuwa mlezi mzuri wa vyama vya siasa na serikali itaendelea kumuenzi na kuendeleza yale aliyoyaanzisha. 
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment