NA MWANDISHI WETU
17th January 2014.
Hata hivyo, amesema uamuzi wa kupita au kutopita kwa Rasimu ya Pili ya Katiba Mpya iliyopendekezwa na tume, utatokana na matakwa ya kidemokrasia ya wabunge watakaounda Bunge la Katiba ambao wanatakiwa kuweka mbele maslahi ya taifa na mshikamano wa Watanzania na uamuzi wa mwisho ambao utatolewa na wananchi wenyewe kupitia kura ya maoni.
Vuai alisema hayo juzi mara baada ya kupokea matembezi ya vijana wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Zanzibar waliotembea umbali wa kilomita sita kuunga mkono hotuba iliotolewa na Rais wa visiwa hivyo, Dk. Ali Mohamed Shein kwenye kielele cha Maadhimisho ya Miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Alisema CCM inatambua kuwapo kwa baadhi ya kasoro katika Muungano wa Serikali mbili ambazo zinaweza kurekebishwa bila ya kuubadili muundo wa Muungano kuwa wa serikali tatu kwani utakuwa na matatizo mengi zaidi ambayo yatapelekea kuvunja kabisa muungano wa kindugu uliopo ambao umedumu kwa miaka 50 sasa.
Alisema katika kipindi cha miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar pande zote mbili zimekuwa zikitegemeana katika masuala mbalimbali huku akitoa mfano wa Tanzania iliposhiriki kwa pamoja vita ya Kagera mwaka 1978 iliyomuangusha nduli Idd Amini.
“Muungano wa Tanganyika na Zanzibar una umuhimu wake kwa amani ya pamoja, utulivu wa ndani na umoja wa kitaifa, hili si jambo la kutaniwa taniwa au kufanyiwa mzaha” aliasa Vuai.
Aidha, Naibu Katibu Mkuu huyo wa CCM Zanzibar aliwahimiza vijana kuhakikisha wanapata vitambulishao vya ukazi na kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa ajili ya kushiriki uchaguzi mkuu mwaka kesho.
CHANZO: NIPASHE
No comments :
Post a Comment