Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, May 29, 2014

AFRICA DAY IN WASHINGTON DC!

   

GALA DINNER YA AFRICAN DAY WASHINGTON, DC YAFANA SANA, MEYA WA DC NDANI YA NYUMBA, TANZANIA NA RWANDA NDIO WAANDAAJI WA MWAKA HUU


Balozi wa kudumu wa African Union Mhe. Amina Salum Ali akiwa kwenye gwaride la bendera wakati hafla ya gala dinner ya African Day iliyofanyika Washington, DC siku ya Jumanne May 27, 2014 katika hotel ya Marriott na kuhudhuriwa na watu zaidi ya 2,000. Afriacam day ya mwaka huu iliandaliwa na Ubalozi wa Tanzania wakishirikiana na Ubalozi wa  Rwanda

Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Liberata Mulamula akiwa kwenye gwaride la bendera wakati wa ufunguzi wa Gala dinner ya African Day siku ya Jumanne May 27, 2014 katika hotel ya Marriott, Washington, DC.
Mabalozi wakisimama kwa nyimbo za taifa za Marekani na African Union.

Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Liberata Mulamula akitoa hotuba ya kuwakaribisha wageni siku ya Jumanne May 27, 2014 siku ya African day iliyoadhimishwa Marriott ya Washington, DC.

Balozi wa Rwanda nchini Marekani Mhe.Mathilde Munkanabana nae akitoa hotuba ya kuwakaribisha wageni.

Balozi wa kudumu wa African Union, Mhe. Amina Salum Ali akitoa hotuba.

Meya wa DC, Mhe.Vincent Gray akitoa hotuba.

Meya wa DC, Mhe. Vinceny Gray akimkabidhi hati ya baraza la jiji la DC Balozi wa kudumu wa African Union, Mhe. Amina Salum Ali ya Jiji la Washington, DC kutambua rasmi siku ya African Day.

Meya katika picha ya pamoja na waheshimiwa Mabalozi wa Rwanda, Tanzania na African Union.

Mwakilishi wa Serikali ya Marekani Mhe. Linda Thomas Greenfield akitoa hotuba.
Mhe. Linda Thomas Greenfield katika picha ya pamoja na waheshimiwa Mabalozi wa Tanzania na Rwanda.

Balozi wa DRC nchini Marekani Mhe. Faida Mitifu akisoma wasifu wa msemaji mkuu wa Afriacan Day Dr. Juma Calestous ambaye ni profesa, Harvard Kennedy School of Gevernment.

Msemaji mkuu wa African Day Dr. Juma Calestous akitoa hotuba yake.

Dr. Juma Colestous katika picha ya pamajoa na waheshimiwa Mabalozi.

Balozi wa Ivory Coast, Mhe. Douda Diabate akitoa hotuba.
Balozi wa Rwanda akisalimia na wageni wakati wa Cocktail Reception.
Balozi wa Tanzania akisalimiana na wageni wakati wa Cocktail Reception.
Picha ya pamoja.

 Kikundi cha utamaduni kutoka Zimbabwe kikitumbuiza kwenye Gala Dinner ya African Day iliyofanyuka siku ya Jumanne May 27, 2014, Marriott Washington, DC.
Juu na chini ni viikundi cha utamaduni kutoka Rwanda kikitoa burudani kwenye siku ya Gala dinner ya Africa Day.
Mhe Balozi Liberata Mulamula Balozi wa Tanzania nchini Marekani akijumuika kwenye ngoma ya utamaduni ya kikundi toka Rwanda.
Mhe. Balozi Mathilde Mukatabana (kati) Balozi wa Rwanda nchini Marekani akijumuika na kikundi cha utamaduni kutoka Rwanda kilipokua kikitoa burudani kwenye Gala dinner ya African Day.


Source: Vijimambo

No comments :

Post a Comment