- Mawaziri kivuli walioachwa katika baraza hilo ni Sylvester Kasulumbay (Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi), Highness Kiwia (Viwanda na Biashara) na Rose Kamili (Kilimo, Chakula na Ushirika).
Dodoma. Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, ametangaza Baraza lake la mawaziri kivuli 28 na naibu mawaziri 12, na kufanya baraza lote kuwa na mawaziri 40.
Katika baraza hilo la mawaziri linalojumuisha wabunge wanaotokana na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), mawaziri 25 wanatoka Chadema, 11 wanatoka CUF na NCCR-Mageuzi ni wanne.
Mawaziri kivuli walioachwa katika baraza hilo ni Sylvester Kasulumbay (Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi), Highness Kiwia (Viwanda na Biashara) na Rose Kamili (Kilimo, Chakula na Ushirika).
Wengine walioachwa na Mbowe akasisitiza kuachwa kwao siyo kwa sababu hawawezi kazi bali ni kutaka kuwa na baraza la mawaziri dogo ni Sabrina Sunga (Naibu Waziri Maji).
Katika Baraza hilo, nafasi ya mnadhimu mkuu wa upinzani Bungeni iliyokuwa ikishikiliwa na Tundu Lissu (Chadema) sasa itashikiliwa na Mbunge wa Tumbe, Rashid Abdalah kutoka chama cha CUF.
Akitangaza baraza hilo Bungeni mjini Dodoma jana, Mbowe alisema Wizara ya Katiba na Sheria imeongezewa majukumu ya Muungano na waziri wake atakuwa ni Lissu na naibu wake ni Abdalah.
Pia amemteua Mbunge wa kuteuliwa na Rais ambaye pia ni Mwenyekiti wa taifa wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia ambaye anakuwa Waziri wa Fedha wakati Naibu wake atakuwa Christina Lissu kutoka Chadema.
Mawaziri Ofisi ya Rais ni Profesa Kulikoyela Kahigi (Utawala Bora-Chadema), Vicent Nyerere (Utumishi-Chadema) na Esther Matiko (Mahusiano na Uratibu-Chadema).
Ofisi ya makamu wa Rais itakuwa na mawaziri wawili ambao ni mchungaji Israel Natse kutoka Chadema atakayeshughulika na Mazingira na Naibu wake atakuwa ni Assah Othman Hamad (CUF).
Mnadhimu wa Upinzani Bungeni ndiye atakayeshikilia pia nafasi ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais anayeshughulikia Mazingira.
Mawaziri katika ofisi ya Waziri mkuu ni Pauline Gekul (Uwekezaji na Uwezeshaji-Chadema), Rajabu Mohamed Mbaruku (Sera, Uratibu na Bunge-CUF) na David Silinde (Tamisemi-Chadema).
Wizara ya Chakula, Kilimo na Ushirika itashikiliwa na Meshack Opulukwa (Chadema), Wizara ya Nishati na Madini atakuwa John Mnyika Chadema na Naibu wake “atakuwa Raya Ibrahim (Chadema).
Kulingana na orodha hiyo, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa itashikiliwa na Ezekiah Wenje (Chadema) na Naibu wake ni Rashid Abdalah kutoka CUF.
Mawaziri wengine na wizara zao kwenye mabano ni Felix Mkosamali (Ujenzi-NCCR-Mageuzi), Magdalena Sakaya (Maji-Cuf), na Moses Machali (Uchukuzi- NCCR- Mageuzi).
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi itaongozwa na Godbless Lema wa Chadema na Naibu wake ni Khatibu Said Haji wa CUF wakati Wizara ya Ardhi, Nyumba na Makazi ni Halima Mdee wa Chadema.
Kwa mujibu wa orodha hiyo, Mbowe amemteua Rose Kamili Sukum kutoka Chadema kuwa Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi wakati Naibu wake atakuwa ni Mkiwa Adam Kiwanga wa CUF.
Wizara ya Maliasili na Utalii itashikiliwa na mchungaji Peter Msigwa (Chadema), Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki imeenda kwa Joseph Selasini (Chadema) na naibu ni Rukia Ahmed Kassim (CUF).
Mbowe pia amemteua Masoud Abdalah Salim wa CUF kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa na Wizara ya Elimu itashikiliwa na Susan Lyimo na Naibu wake ni Joshua Nasari wote toka Chadema.
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imeenda kwa Dk Gervas Mbassa na Naibu wake ni Conchesta Rwamlaza wote wa Chadema. David Kafulila (NCCR) ameteuliwa Waziri wa Viwanda na Biashara.
Katika baraza hilo la mawaziri, Injinia Habib Mnyaa wa CUF ameteuliwa kuwa Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia wakati Lucy Owenya kutoka Chadema akiteuliwa kuwa naibu wake.
Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto imeenda kwa Baruan Salum Khalfan wa CUF na Naibu wake ni Subreena Sungura wa Chadema. Cecilia Paresso wa Chadema anakuwa Waziri wa Kazi na Ajira.
Wizara ya Habari, Vijana na Michezo imeendelea kushikiliwa na Joseph Mbilinyi wa Chadema.
Akizungumza na wanahabari, Mbowe alisema wakati katika Baraza la Mawaziri la Serikali ya CCM, wanaume ni 36 na wanawake 15, wao upinzani wanaume ni 26 na wanawake ni 14.
Hali kadhalika Mbowe alisema wakati Baraza zima la mawaziri la Serikali ya CCM likiwa na mawaziri kamili 28 na manaibu 22, wao Baraza lao Kivuli lina mawaziri kamili 28 na naibu mawaziri 12.
Alisema nafasi ya Naibu Kiongozi wa Upinzani Ubungeni iliyokuwa ikishikiliwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe itantangazwa baadaye
Habari hii imeandikwa na Daniel Mjema, Sharon Sauwa na Fidelis Butahe
Source: Mwananchi
Hili Baraza ni hafifu na halitotufikisha popote.
ReplyDeletePia ni kubwa kama la CCM. Mawaziri 20 tu wangetosha!