Mhe Mohamed Raza Dharamsi Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Mkoa wa Kusini Unguja kumbe nae ni FISADI mkubwa anaejificha nyuma ya shati la kijani. Dawa ya kuwaondoa mafisadi nchini ni kuwapiga risasi hadharani Mnazi Mmoja!
Waziri wa Fedha Zanzibar amshikia Raza bango la kodi
Na Mwinyi Sadallah, Mwananchi
Posted Juni28 2014 saa 10:51 AM
Posted Juni28 2014 saa 10:51 AM
KWA UFUPI
- NI kutokana na kudai kampuni ya ZAT ambayo mwenyekiti wake ni Raza kuikosesha mapato SMZ yatokanayo na gawio la faid
Zanzibar.Mfanyabiashara maarufu wa Zanzibar, Mohamed Raza Dharamsi anadaiwa kodi inayotokana na gawio la faida kwa muda wa miaka 16 na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) kupitia Kampuni ya ZAT inayotoa huduma za viwanja vya ndege visiwani Zanzibar, imefahamika.
Hayo yalielezwa na Waziri wa Fedha, Omar Yussuf Mzee katika kikao cha Baraza la Wawakilishi wakati akichangia Bajeti ya Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano baada ya baadhi ya wajumbe kutaka kujua kwa nini kampuni ya ZAT hailipi kodi kwa wakati mwafaka ikiwamo gawio la faida ya Serikali la asilimia 5 kutokana na mapato na faida.
Waziri Mzee alisema tayari amekwishaagiza watendaji wa Wizara ya Fedha kwenda kupitia hesabu za kampuni ya ZAT ili kujua faida waliyoipata kwa muda wa miaka 16, ili SMZ ijue inaidai kampuni hiyo kiasi gani cha fedha itokanayo na faida ya utoaji wa huduma katika viwanja vya ndege.
Hata hivyo, waziri huyo alisema viongozi dhamana wa Fedha waliopita ndiyo waliochangia kwa kiasi kikubwa kwa kampuni ya ZAT kutolipa kodi kwa wakati kwa vile walishindwa kusimamia ipasavyo majukumu yao.
Alisema baada ya kukabidhiwa Wizara ya Fedha mwaka 2010 alilazimika kumwita Mwenyekiti wa Kampuni ya ZAT, Mohamed Raza Dharamsi ambaye pia Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Mkoa wa Kusini Unguja, na kumtaka aeleze ni kwa nini kampuni yake imekuwa haiilipi serikali gawio la asilimia 5 na kuikosesha mapato SMZ.
Aidha, alisema baada ya kuanza kufuatilia, SMZ imefanikiwa kukusanya Sh890 milioni kutokana na kumpa siku tano Raza kuhakikisha analipa gawio la Serikali na awamu ya kwanza ZAT ililipa Sh400milioni na baadaye Sh450 milioni na kuwataka watendaji kuangalia ni kiasi gani bado kinadaiwa katika miaka 16 mbali na kiwango kilicholipwa.
Waziri Mzee alisema kati ya fedha hizo gawio la Serilali alilipa Sh440 milioni ikiwa ni kuanzia mwaka 2012 hadi 2013 na kodi nyinginezo Sh450 milioni huku akiwahimiza watendaji kupitia kwa umakini hesabu zote za miaka ya nyuma bila kungoja.
No comments :
Post a Comment