Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, June 20, 2014

Watoto wa Wanamapinduzi watambiana kuwania Kiembesamaki


Mahmoud-Thabit-Kombo.PICHA|MAKTABA 
Na Mwinyi Sadallah, Mwananchi

Posted  Alhamisi,Juni19  2014
KWA UFUPI
Majigambo haya yanaonyesha wazi mwaka 2015 kutakuwa na mchuano mkali Jimbo la Kiembesamaki.

Zanzibar.
 Wiki iliyopita mtoto wa muasisi wa ASP, Mansoor Yussuf Himid alitangaza kujiunga na Chama cha Wananchi (CUF) baada ya kuondolewa CCM kwa tuhuma za kukiuka maadili.
Uamuzi wake wa kujiunga na CUF uliamsha hisia tofauti katika mustakabali wake kisiasa, kiasi cha mwakilishi wa Mji Mkongwe, Ismail Jussa Ladhu kujitolea kumuachia kiti cha jimbo hilo iwapo angetaka kuendelea na siasa.
Lakini Mansoor ameibuka na kusema kuwa anataka kuwania kiti cha Jimbo la Kiembesamaki, uamuzi ambao utampambanisha na Mahmoud Thabit Kombo ambaye ni mtoto wa muasisi mwingine wa ASP, Sheikh Thabit Kombo Jecha kwenye Uchaguzi Mkuu ujao.
Wakiwa vyama hasimu, tayari watoto hao wameanza kutambiana na kila mmoja anajivunia mtaji wa historia ya mzazi wake katika siasa za Zanzibar.
Wakati Mahmoud akiwa ni mtoto wa Sheikh Thabit Kombo Jecha aliyekuwa katibu mkuu wa ASP, Mansoor ni mtoto wa aliyekuwa mkuu wa jeshi la ukombozi la Zanzibar, Brigedia Yussuf Himid Maftah na mmoja kati ya watu 14 walioshiriki mapinduzi ya Januari 12, mwaka 1964.
Mahmoud na Mansoor wote wamewahi kuwa mawaziri katika serikali ya Rais Amani Karume, wajumbe wa NEC ya CCM na wawakilihi wa majimbo ya Mpendae na Kiembesamaki kabla ya Mahmoud kuhamia Kiembesamaki baada ya kufukuzwa uanachama wa CCM kutokana na kwenda kinyume na maadili.
Mapema wiki iliyopita, Mansoor alitangaza kujiunga CUF na kuahidi kuwania kiti cha Kiembesamaki.
Mahmoud alisema jimbo hilo si miliki ya upinzani na kwamba anamkarabisha mgombea yeyote ili kuchuana naye na kusema atatoka kwa aibu.
Mahmoud amesikika akisema hana shaka na mikogo ya wapinzani na kueleza katika uchaguzi mdogo uliomalizaka Februari mwaka huu, CCM ilishinda kwa asilimia 78 na kwamba mwaka 2015 itashinda kwa asilimia zaidi ya 90.
Manssor amekataa katakata ombi la mwakilishi wa Mji Mkongwe, Ismail Jussa Ladhu aliyesema yuko tayari kumwachia kiti hicho na kusema ikiwa ataamua kurudi tena kwenye ulingo wa siasa atawania katika Jimbo la Kiembesamaki ambako amewekeza na anadai anakukubalika.
Akieelezea mpango wa kuwania kiti hicho, Mansoor anasema anapata matumaini kutokana na kundi kubwa la vijana na wazee kuwa nyuma yake.
Anasema alivyolitumikia jimbo hilo akiwa CCM, utendaji wake unafahamika kwa wakazi wote.
Hata hivyo, maelezo hayo yamebezwa na Mahmoud anayesema kwamba katika kipindi kifupi tangu kuchaguliwa kwake, tayari ametekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM kwa vitendo na hafikirii kama anaweza kupigwa mwereka na Mansoor.
Pepo za siasa zikionekana kuvuma kwa nguvu mpya katika jimbo hilo, kwa wakati huu kila mmoja anaonekana kutumia nguvu zake kisiasa.
Wote pia wanatumia umaarufu wa wazazi wao katika mapinduzi ya Zanzibar mwaka 1964 na pia nguvu za vyama vyao.
Mzee Thabit Kombo akiwa na heshima ya kisiasa hasa baada ya kuziunganisha jumuiya za Washiraz na Waafrika mwaka 1957, Brigedia Himid ndiye aliyekuwa kinara wa mipango na kufanikisha Mapinmduzi ya Zanzibar.
Ni vigumu kuizungumzia siasa ya Zanzibar hasa katika ujenzi wa ASP na mapinduzi ya Zanzibar na kuyaacha majina na wazee hao wawili ambao ni wazazi wa Mahmoud na Mansooor.
Sasa watoto wao wamepanda kwenye majukwaa ya vyama tofauti na hasimu katika siasa huku Mansoor akitumia sera za CUF na Mahmoud akibaki katika chama cha asili ya baba yake, sasa CCM.
Mansoor ametaganza kuwa mpango wake kwa sasa ni kuhakikisha CUF inachukua pia kiti cha urais Zanzibar. Anaamini kwa kuongeza mtaji wake wa siasa atamuwezesha Katibu Mkuu wa CUF, Seif Sharif Hamad kuingia Ikulu mwaka 2015.
Mahmoud anasema hakuna la kumzuia tena Dk Ali Mohamed Shein asishinde uchaguzi mkuu ujao na kumaliza ngwe yake ya miaka 10. Mahmoud anawataka wananchi kuendelea kuyatetea mnapinduzi ya mwaka 1964, lakini Mansoor anashangaa iweje wanaojinasibu kudumisha mapinduzi, wanahubiri ubaguzi?
utengano, ukabila na kutumia rangi kama mtaji wa kisiasa.
Nini kitatokea kati ya watoto hao wawili wa waasisi waliopanda katika jahazi la siasa wakitofautiana itikadi za vyama? Hili ni jambo la kusubiri wakati na muda ili kujua mbichi na mbivu mwaka 2015.
.

No comments :

Post a Comment