Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, June 8, 2014

Wawakilishi waikataa Bajeti ya Wizara ya Afya

Na Mwinyi Sadallah, Mwananchi

Jumapili,Juni8  2014.
KWA UFUPI
Alisema bajeti hiyo sasa itarudi katika Kamati ya Wanawake na Watoto na ustawi wa jamii husika ili ikae tena na Wizara ya Afya pamoja na watendaji wa Wizara ya Fedha kwa lengo la kurekebisha upungufu huo kabla ya kuendelea kujadiliwa tena ndani ya baraza.
Zanzibar. Baraza la Wawakilishi Zanzibar limeamua kuondoa Bajeti ya Wizara ya Afya baada ya wajumbe wa baraza hilo kuipinga kwa madai kuwa matumizi yaliyopendekezwa hayajazingatia kuondoa kero zinazoikabili sekta ya afya.
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Pandu Ameir Kificho alisema baraza limefikia uamuzi huo baada ya wajumbe wengi kubaini upungufu mkubwa wa mgawanyo wa fedha katika bajeti ya wizara hiyo mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Kificho alitoa ufafanuzi huo na kusema wajumbe wamebaini kiasi kidogo cha fedha zilizotengwa kwa ajili ya wizara hiyo mwaka huu, pia kuna vitengo vimetengewa kiwango kidogo cha matumizi katika mwaka huu wa fedha.
Alisema iwapo mapendekezo ya bajeti hiyo yatapitishwa na baraza bila ya kufanyika kwa marekebisho na kuzingatia vipaumbele kutachangia kupunguza ufanisi wa utendaji na utoaji wa huduma kwa wananchi wa Unguja na Pemba.
Alisema bajeti hiyo sasa itarudi katika Kamati ya Wanawake na Watoto na ustawi wa jamii husika ili ikae tena na Wizara ya Afya pamoja na watendaji wa Wizara ya Fedha kwa lengo la kurekebisha upungufu huo kabla ya kuendelea kujadiliwa tena ndani ya baraza.
Tukio hili linaonyesha jinsi Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi walivyo makini katika kuhakikisha bajeti ya Serikali inakuwa kwa masilahi ya wananchi na si vinginevyo.
Hivi karibuni, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi walipatiwa mafunzo kuhusu uchambuzi wa Bajeti kupitia Mradi wa Kuimarisha Vyombo vya Kutunga Sheria (LSP) na umakini huo wa wajumbe katika kuijadili Bajeti ya Wizara ya Afya unathibitisha namna mafunzo hayo yalivyosaidia kuwajengea uwezo katika eneo hilo
.

No comments :

Post a Comment