dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, August 5, 2014

BALOZI MULAMULA TAFADHALI ELEZA UKWELI!!!

UBALOZI WA TANZANIA NCHINI MAREKANI BADILIKENI


Balozi wa Tanzania Marekani Mhe Liberata Mulamula - tafadhali eleza ukweli!
Mimi kama Mtanzania naandika hapa kuwaomba watumishi wa Ubalozi wa Tanzania Washington DC ubadilike kuwa na hali ya ujamaa.Sisi kama Watanzania tunatakiwa kuwa na umoja kwenye kila jambo.Ubalozi mnatakiwa kumshirikisha kila Mtanzania hususan katika shughuli za mikutano ya kijamii.
Huu ujio wa Raisi Kikwete na mwaliko wa kuwaita Watanzania siku chache kabla ya huo mkutano umeonyesha wazi jinsi gani mnavyowadharau Watanzania wengine ambao wapo mbali kidogo na DMV au State za mbali.Wengi wanajiuliza hivi Ubalozi wa Tanzania USA ni wa DMV tu?

Mualiko wa Rais hauwagi wa surprise sasa iweje nyie ndugu zetu wa Ubalozi mtualike siku chache kabla.nyie kama wakazi wa hapa USA mnajua wazi kuwa mtu anahitaji atleast 3 weeks au mwezi mzima ili aweze omba ruhusa kazini au aweze kujitayarisha kivyake kuja kuhudhuria huo mkutano wa Watanzania wa kuonana na Rais wao.kila mtanzania ana haki hio na Ubalozi upo hapa kwa ajili ya kila Mtanzania sio tu watanzania wa DMV tu.Sasa kipi kilichawapa ugumu wa kualika mapema?Hata huo msafara wa Rais ulihitaji muda wa more than two weeks for visa processing etc.

Rais Kikwete, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernad Membe, Balozi wa Tanzania Marekani Mhe Liberata Mulamula na Bi Rose Jairo, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora wakijadiliana jambo meza kuu hivi majuzi Marekani.

Kingine ni kuhusu huo mwaliko wa wajasiriamali wa DMV kukutana na Mama Salma, hivi naomba niwaulize lini mtaacha ubinafsi na ujamaa wa kuitana wenyewe kwa wenyewe kuja msikia au munaona First Lady wetu.Hivi kwani Watanzania wengine au wanawake wengine ambao ni wajasiriamali pia hawana haki?Sasa mbona hamjaalika kila mjasiriamali mwanamke?wa hapa USA. Hao waliohudhuria ni wanawake wachache tu ambao mme wachagua kiujamaa jamaa na kiubinafsi.
Mwisho mimi kama Mtanzania mwenzenu naomba mbadili hii tabia ambayo inagawanya watanzania na kuwafanya kujisikia vibaya kuwa wamebaguliwa kisha kukata tamaa kabisa na ubalozi wetu.

Ni mimi Buhite Jabry

No comments :

Post a Comment