dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, August 5, 2014

Zanzibar wataka uchumi wao usiingiliwe

   

     


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein  
Na Mwinyi Sadallah, Mwananchi

Posted  Jumanne,Agosti5  2014
KWA UFUPI
Mapendekezo hayo yamewasilishwa kwa Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein, Spika wa Baraza la Wawakilishi, Pandu Ameir kificho, Makamu wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif Sharif Hamad na Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Iddi.

Zanzibar. Kamati ya Kuwaunganisha Wazanzibari imependekeza mambo tisa yanayopaswa kutetewa na kuzingatiwa na wajumbe wa Bunge la Katiba ikiwamo Zanzibar kupewa mamlaka kamili ya kusarifu na kushughulikia uchumi wake bila ya kuingiliwa na taasisi yoyote katika mfumo wa Muungano.
Mapendekezo hayo yamewasilishwa kwa Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein, Spika wa Baraza la Wawakilishi, Pandu Ameir kificho, Makamu wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif Sharif Hamad na Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Iddi.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa kamati hiyo ambayo iliundwa na Taasisi ya Utafiti na Sera za Umma (ZIRRP), Ali Abdullah Suleiman alisema lazima Katiba Mpya itoe haki na hadhi sawa kwa nchi mbili zilizoungana kama Ibara ya 64(5) ya Rasimu ya Katiba inavyopendekeza ili kuondokana na upande mmoja wa muungano kuonekana unanyonywa kama ilivyo sasa.
Pia wametaka Zanzibar ipewe mamlaka ya kuanzisha Benki yake (State Bank) pamoja na kuwapo kwa Benki Kuu ya Tanzania kama inavyopendekezwa katika masharti ya Ibara ya 234 ya Rasimu ya Katiba inayoanza kujadiliwa leo.“Mambo mengine tuliyopendekeza kuhakikisha Zanzibar inapata mamlaka ya kujiunga na mashirika ya kikanda na kimataifa kama vile Fifa, OIC, SADC, EAC, Unesco, Who na Fao,” alisema mwenyekiti huyo.
Kamati hiyo ya kuwaunganisha Wazanzibari imesema wakati umefika Rais wa Tanzania awe anapatikana kwa utaratibu wa zamu baina ya pande mbili za Muungano na Rais wa Zanzibar arejeshewe hadhi yake ya kuwa Makamu wa Rais wa Muungano.
Alisema baada ya kamati kuchambua kwa kina, chimbuko la mgawanyiko uliojitokeza wa Bunge la Katiba wamebaini iwapo mapendekezo hayo yatazingatiwa yatajenga umoja na masilahi ya Zanzibar kuonekana katika Katiba Mpya.
Hata hivyo, alisema waraka huo umependekeza Zanzibar kuanzisha idara yake ya polisi, pamoja na kuwapo kwa jeshi la polisi la Muungano kama Ibara ya 232 (1) (2) ya Rasimu ya Kwanza ya Katiba ilivyokuwa imependekeza na kuhakikisha Zanzibar inapata mamlaka yake ya kuanzisha idara ya usalama wa Taifa pamoja na kuwapo kwa idara kama hiyo ya Muungano.
Mapendekezo mengine ni kuhakikisha kuwa nafasi zote za ajira katika utumishi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zinatolewa kwa utaratibu wa uwiano kama ilivyoshauriwa na kupendekezwa katika Rasimu ya Ibara ya 185(1) na (2) ili kuweka usawa baina ya pande mbili za Muungano.
Kamati hiyo imetaka wabunge wa kundi la Ukawa warudi bungeni wakajadili hoja kupitia rasimu iliyowasilishwa ili wananchi wapate fursa ya kuwasikiliza kabla na wao kupata fursa ya kuamua katiba waitakayo kupitia kura ya maoni

No comments :

Post a Comment