Silaha alizokamatwa nazo Mhe Mansoor ambazo zilikuwa zinazo ruhsa.
Na Mwinyi Sadallah, Mwananchi.
Na Mwinyi Sadallah, Mwananchi.
KWA UFUPI
Kesi hiyo iliahirishwa jana mbele ya Naibu Mrajis wa Mahakama Kuu Yesaya Kayange hadi Septemba 29, huku mshtakiwa Abdulrahman Thani Matar(39) na Mohamed |Thani Matar(37) wakiwa ndani kutokana na shtaka hilo kutokuwa na dhamana.
Zanzibar - Kesi ya mauaji dhidi ya raia wawili wa Ufaransa imekwama kuanza kusikilizwa kwa miezi minane sasa, baada ya upande wa mashtaka kuendelea na madai ya kutokamilika kwa ushahidi wa kesi hiyo.
Kesi hiyo iliahirishwa jana mbele ya Naibu Mrajis wa Mahakama Kuu Yesaya Kayange hadi Septemba 29, huku mshtakiwa Abdulrahman Thani Matar(39) na Mohamed |Thani Matar(37) wakiwa ndani kutokana na shtaka hilo kutokuwa na dhamana.
Mwendesha mashtaka wa Serikali Ali Yusuph Ali alimweleza mrajis wa mahakama hiyo kuwa upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika na kuomba mahakama kupanga tarehe nyingine ya kusikilizwa kwa kesi hiyo.
Kwa mujibu wa hati ya mashtaka watuhumiuwa hao wanadaiwa kumuua Francios Denis Robert na mkewe Brigitte Meny katika Kijiji cha Matemwe Minazi Mirefu kati ya Desemba 2013 saa 5:50 na saa 7:00 katika Wilaya ya Kaskazini A Unguja.
Wakati huohuo kesi inayomkabili Waziri wa zamani wa SMZ, Mansour Yusuph Himid anayekabiliwa na shtaka la kupatikana na silaha ya moto pamoja na risasi 407 kinyume na sheria ya silaha na risasi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeahirishwa tena baada ya upande wa mashtaka kudai kuwa upelelezi bado haujakamilika.
Waziri huyo wa zamani yupo nje baada ya kuachiwa kwa dhamana na Jaji Abraham Mwampashi ambaye alisema hakuna makosa ya jinai yasiyokuwa na dhamana Zanzibar na kumwachia kwa masharti ya fedha taslimu milioni 3, wadhamini wawili wenye vitambulisho vinavyotambulika waliosaini bondi ya milioni tano kila moja, kuwasilisha hati ya kusafiria mahakamani na kutosafiri bila ya ruhusa ya mahakama.
Kesi hiyo ambayo ilitajwa mbele ya Naibu Mrajis Yesaya Kayange imeahirishwa hadi Septemba 30 mwaka huu.
.
.
Mwenyekujua jamani atueleze ni lini uchaguzi wa Kiembe Samakai na kama Mheshimiwa Mansour anaweza kushiriki.
ReplyDelete