WAPIGANAJI wa JWTZ Kisiwani Pemba, wakibeba baadhi ya Vyakula vilivyotolewa na Uongozi wa JWTZ Tanzania, kwa ajili ya kusaidia Vituo vya watoto mayatima kisiwani Pemba na kumkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mhe;Mwanajuma Majid Abdalla kwa lengo la kuvigawa katika vitu hivyo.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
MKUU wa Mkoa wa Kusini Pemba, Mhe:Mwanajuma Majid Abdalla akipoke msaada wa chakula kutoka kwa uongozi wa JWTZ Tanzania, kwa lengo la kupatiwa Vituo vya watoto mayatima, ikiwa ni maadhimisho ya Miaka 50 tokea kuanzishwa kwa jeshi hilo nchini.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
MKUU wa Utawala wa Bregedia ya 101 Zanzibar, Meja Mohammed Suleiman Ali katikati, akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa kusini Pemba Mhe:Mwanajuma Majid Abdalla, msaada wa mafuta ya kupikia kwa ajili ya Vituo vya kulelea watoto mayatima kisiwani Pemba, hafala iliyofanyika katika kiwanja cha Tenis Chake Chake Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
MKUU wa Mkoa wa kusini Pemba, Mhe:Mwanajuma Majid Abdalla mwenyedira, akiwa katika picha ya Pamoja na wapigani wa JWTZ Tanzania, mara baada ya kukabidhiwa msaada wa Vyakula kwa ajili ya Vituo vya Watoto Mayatima kisiwani Pemba, ikiwa ni maadhimisho ya miaka 50 tokea kuanzishwa kwa Jeshi hilo Tanzania.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
Chanzo: ZanziNews
No comments :
Post a Comment