airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, September 19, 2014

Mahujaji wa Zanzibar Waondoka leo.

Kaimu Mkurugenzi Masoko wa Benki ya Watu wa Zanzibar Ndg. Seif Suleiman akiwa na Maofisa wa PBZ wakiandaa maji na biskuti kwa ajili ya Mahujaji na Wananchi waliowashindikiza Ndugu zao katika uwanja wa ndege wa Zanzibar PBZ imemeto huduma hiyo kwa wananchi waliofika katika viwanja hivyo.
Wananchi na Waumini wa dini ya Kiislam Zanzibar wakiwa katika viwanja vya uwanja wa ndege Zanzibar kuwashindikiza Mahujaji wanaokwenda Mecca kukamilisha moja ya nguzo tano za Kiislam kwenda makka kuhuji.
Ustadh Kizito akitowa maelezo kwa Mahujaji wanaofika katika Uwanja wa Ndege wa Zanzibar taratibu za kukamilisha safari yao ya kwenda Makka kuhiji 
Jumuiya ya Istiqama ya kusafirika Mahujaji Tawi la Zanzibar, wakifanya taratibu kwa wahujaji wake wanaokwenda Makka kuhiji, jumla ya mahujaji 381, wameondoka leo kupitia taasisi tatu Zanzibar.
Mmoja wa Mahujaji akiagana na Ndugu na Jamaa wakati wa kuaza safari yao leo kwenda Makka kukamilisha nguzo tano za Kiislam, wameondoka leo mchana kwenda Saudi Arabia kukamilisha ibada hiyo.
Waumini wa Dini ya Kiislamu wakimuombea dua Hujajaji ndugu yao anaekwenda Makka kuhiji
Mahujaji wa Wanawake wakisoma muongoza wa kushiriki Ibada ya Hijja, wakiwa katikac viowanja vya Ndege Zanzibar kabla ya kuondoka leo mchana.
Kaimu Mkurugenzi Masoko Benki ya Watu wa Zanzibar Ndg. Seif Suleiman, askigawa biskuti kwa wananchi waliofika kuwaanga ndugu zao wanaokwenda hija.
Mahujaji wa Zanzibar wakiwasalimia na kuwaaga ndugu zao wakati wakiondoka Zanzibar leo mchana, kuelekea Makka kwa ajili ya kuhija. 




No comments :

Post a Comment