Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, September 2, 2014

Mkasi | SO9E11 with Zitto Kabwe

  
September 24, mwaka 1976 ni tarehe muhimu kwenye historia ya siasa na harakati Tanzania! Ni siku alizaliwa Ndugu Zitto Zuberi Kabwe. Kwa sasa ni Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), nafasi anayoishikilia tangu mwaka 2005.

Zitto, hakuanza harakati na uongozi baada ya kuingia rasmi kwenye siasa. Katika kipindi cha mwaka 2002-2003, alishika nafasi ya Katibu Mkuu wa Baraza la Wanafunzi la Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam. Mara baada ya kuhitimu katika Shahada ya Sanaa katika Uchumi, alikwenda nchini Ujerumani ambako alikuwa akisomea masuala ya Masoko ya Kimataifa, na wakati huo huo akisimamia Kurugenzi ya Masuala ya Kimataifa ya Chadema. 

Mnamo mwaka 2005, Zitto aliamua kujiingiza kwenye kinyang'anyiro cha Uchaguzi na alifanikiwa kutwaa kiti cha Kigoma Kaskazini, nafasi aliyofainikiwa kuitetea tena katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.

Katika nafasi yake kama Mbunge alipata pia kutumikia Taifa kama Mjumbe wa Tume ya Rais ya Kupitia Sekta ya Madini, Kamati ya kuharakisha Mchakato wa Shirikisho la Kisiasa la Afrika Mashariki kati ya nyingi. Kwa sasa ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali. Pia amekuwa akisikika sana katika anga za Rasilimali hasa akiongelea kwa ukali mapungufu katika Mikataba ya Uchimbaji wa Madini na Gesi nchini.

Hivi karibuni Zitto alivuma sana pale Chama chake kilipomtuhumu kwa Usaliti na kuanzisha vuguvugu la kumvua uanachama, juhudi ambazo kwa sasa zimesimama kutokana na pingamizi la kisheria lililowekwa na upande wake. Pamoja na hayo kumekuwa na fukuto la fununu za hapa na pale kuwa anaweza kuhama chama, na kuhamishia harakati zake katika chama kingine....kipya au kilichopo tangu zamani! 

Mwaka huu 2014 haukuwa mzuri sana kwani akiwa katikati ya tuhuma za usaliti wa chama, Zitto alipatwa na Msiba wa Mama Yake kipenzi, na mhimili wake mkuu wa faraja na hamasa. 

Zitto hakutueleza sana kuhusu maisha yake binafsi, ila kama alivyonukuliwa katika mahojiano na Mkasi, alitumia msemo maarufu toka kwenye wimbo wa Hamis Mwinjuma (Mwana FA) maarufu kama "Bado Nipo Nipo", akimaanisha bado hajaoa. 

Mengi zaidi, endelea kumsikiliza na kutazama show yetu siku alipoamua kuja kwenye Kijiwe cha Mkasi kuongea na Wanamkasi!


Furahia!

L•O•V•E

No comments :

Post a Comment