Written by Zdaima // 23/09/2014
Kwa mujibu wa chanzo chetu, ni mara nyengine tena Zanzibar IMEBANWA na muungano kupitia kadhia ya TCAA.
TCAA – Tanzania Civil Aviation Authority imenyima vibali vya shirika moja la ndege linalojishughulisha kubeba watalii wa moja kwa moja kutoka Italy hadi Zanzibar.Mpasha habari wetu ameeleza kwamba ni karibu wiki sasa TCAA imenyima vibali charted flight sita kati ya kumi ambazo zikijushughulisha na huduma hizo. Chanzo kinasema TCAA imefuta vibali hivyo baada ya shirika hilo kushindwa kulipia ada mpya na kuiita utaratibu wa malipo ya zamani kuwa hauna maslahi na TCAA bila kuishirikisha SMZ katika maamuzi hayo. Chanzo kimeeleza kuwa TCAA imeongeza ada ya malipo kutoka dola 1000 za mkataba wa malipo kwa kila ndege kwa wiki ambapo inakisiwa kila ndege ilikuwa inakuja zaidi ya mara tatu Zanzibar na kufikia dola 1500 kwa kila ruti moja jambo lililopelekea wamiliki kushindwa.
Chanzo kinaarifu kuwa maamuzi hayo hayakuishirikisha Zanzibar na imeathiri mtiririko wa mapato ya utalii hasa katika kipindi hiki cha high season ya utalii “…kumekuwa na desturi hii kila ifikapo high seasons kunakuwa na mambo haya sijui tuite hujuma ama vipi?” alisikika ofisa mmoja wa utalii akieleza kwa mpasha habari wetu.TCAA – Tanzania Civil Aviation Authority imenyima vibali vya shirika moja la ndege linalojishughulisha kubeba watalii wa moja kwa moja kutoka Italy hadi Zanzibar.Mpasha habari wetu ameeleza kwamba ni karibu wiki sasa TCAA imenyima vibali charted flight sita kati ya kumi ambazo zikijushughulisha na huduma hizo. Chanzo kinasema TCAA imefuta vibali hivyo baada ya shirika hilo kushindwa kulipia ada mpya na kuiita utaratibu wa malipo ya zamani kuwa hauna maslahi na TCAA bila kuishirikisha SMZ katika maamuzi hayo. Chanzo kimeeleza kuwa TCAA imeongeza ada ya malipo kutoka dola 1000 za mkataba wa malipo kwa kila ndege kwa wiki ambapo inakisiwa kila ndege ilikuwa inakuja zaidi ya mara tatu Zanzibar na kufikia dola 1500 kwa kila ruti moja jambo lililopelekea wamiliki kushindwa.
Taarifa zinazidi kudokeza kuwa licha ya jitihada za wizara husika za fedha, miundombinu na vitengo vya utalii- Zanzibar na wenzao wa bara bado hadi jana mchana 22/9/2014 hakukuwa na taarifa za utatuzi wa kadhia hii. Taarifa zinaeleza kuripotiwa kadhia hii kwa ofisi ya makamo wa pili wa rais SMZ.
ATHARI
akitoa uchambuzi ofisa mmoja wa utalii alieleza kuwa jaalia kila charter moja ikiwa inaleta watalii 4 mara 3 kwa wiki kwa chata kumi ni sawa na watalii 120. kwa wiki hivi SMZ imekosa mapato kiasi gani kwa wiki na kwa siku? vipi mahoteli na kukosa hotel levy, transport levy na kwa upande wa tour operators?, wafanyabiashara ndogo ndogo na kadhalika inakuwaje.
akitoa uchambuzi ofisa mmoja wa utalii alieleza kuwa jaalia kila charter moja ikiwa inaleta watalii 4 mara 3 kwa wiki kwa chata kumi ni sawa na watalii 120. kwa wiki hivi SMZ imekosa mapato kiasi gani kwa wiki na kwa siku? vipi mahoteli na kukosa hotel levy, transport levy na kwa upande wa tour operators?, wafanyabiashara ndogo ndogo na kadhalika inakuwaje.
Zdaima.
Chanzo: Mzalendo
No comments :
Post a Comment