Bw. Othman
Na Mwinyi Sadallah, Mwananchi
Zanzibar. VIongozi wa kisiasa na wanasheria wamegawanyika visiwani Zanzibar kufuatia uamuzi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar(SMZ), Othman Masoud Othman kuamua kujiuzulu katika kamati ya kuandika Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Othman alichukua uamuzi wa kujiuzulu akilinda na kutetea msimamo wake wa kutaka mfumo wa Muungano wa Seriikali tatu uliokuwa umependekezwa katika rasimu ya awali ya Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ya Jaji Joseph Warioba, tofauti na marekebisho yaliyofanywa na Bunge la Katiba chini ya Mwenyekiti wake Samuel Sitta.
Rais wa Chama cha Wanasheria Zanzibar, Awadhi Ali Said alisema uamuzi aliouchukua mwanasheria huyo ni muafaka kwa vile rasimu inayojadiliwa hivi sasa msingi wake mzima umevunjwa.
Alisema kwa kuwa Mwanasheria Mkuu wa SMZ katika mamabo ya katiba na sheria kwa msingi huo Zanzibar imepoteza uwakilishi katika uandikaji wa katiba mpya.
Alisema suala la kujiuzulu kwake si jambo jepesi kwa vile kuingia kwake kwenye Bunge la Katiba kulitokana na wadhifa wake na hakuiingia kama Masoud ila ni mwanasheria wa Serikali ya M,apinduizi Zanzibar aliyeteuliwa na Rais wake.
Alisema kwa hali ilivyosasa inastahili kwa wabunge wote kutoka Zanzibar wanapaswa kujitoa na kurejea nyumbani kutokana na msingi mzima kuvurugwa na kupoteza matumaini baada ya kuingizwa mambo ambayo hayakuwamo.
No comments :
Post a Comment