Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, September 9, 2014

WE ASK AGAIN: WHITHER ARE WE BOUND IN DMV???

Solomon akiuliza maswali huku Saidi Mwamendi akimuwekea pingamizi ambalo lilitupiliwa mbali na NGUVU YA UMMA   



  Vijana wanao jiita Nyarugusu (Idd Green Guard) wakimvamia Dotto Mallongo

  FULL: MREJESHO: NINI KILITOKEA KWENYE MKUTANO MKUU BATILI ATC-METRO/DMV USA September 7, 2014

  • Nje ya wanachama 586 mahudhurio ni wanacham 28
  • Maswali ya Solomon Cris yavunja mkutano kwa muda
  • Vijana wanao jiita Nyarugusu (Idd Green Guard) wataka kumshambulia Solomon na Dotto; yote haya yapo kwenye video chini hapa

    Mkutano ulianza kwa maswali ya hapa na pale na ndipo mwanachama wa jumuia Ndg. Solomn Cris alipo omba fursa ya kuuliza maswali.  Solomon aliruhusiwa kuuliza maswali huku Ndg Saidi Mwamendi akipinga Solomon asiulize maswali.  Watu ukumbini walilipuka na kumwambia Saidi muache Solomn aulize swali kwani kuna wengine wameruhusiwa waulize maswali kwa nini unamuwekea pingamizi Solomon?  Msukumo kutoka kwa wanachama ulikuwa mkubwa na Saidi alishindwa kwa nguvu ya wanachama.  Solomoni aliruhusiwa kuuliza swali.  Solomon aliuliza maswali mawili ya kimsingi kabla ya kuendelea kwa mkutano.  Masali hayo ni kama yafuatayo
1) Huku akiwa na katiba ya jumuia mkononi, Solomni alianza kwa kujitambulisha; “Naitwa Solomon Cris ni mwanachama hai wa jumuia na nina tekeleza haki yangu kama mwanachama, ninauliza swali; katiba yetu inatuambia mkutano mkuu hufanyika kwenye uchaguzi mkuu ambapo uongozi unao achia madaraka hutoa report ya fedha na miradi mbalimbali ya jumuia, lakini cha ajabu haya hayakufanyika kwenye uchaguzi. 
Swali; kwa nini report ya fedha haikutolewa siku ya uchaguzi kama katiba inavyo sema? Kawaida report ya fedha siku ya uchaguzi huwa ina “determine” matokeo ya uchaguzi.  Naomba nijibiwe kwa nini ile report haikutolewa siku ile ya uchaguzi na inatolewa leo hii? Sijui nani atanijibu, lakini mwenyekiti wa Board of Trustee, Hamza Mwamoyo, ndiye ninaye mtambua kama kiongozi halai hapa labda atanijibu.
2) Solomon aliuliza swali la pili kwa kusema; “Katiba inatuambia na ninayo hapa mkononi kuwa, ili mkutano mkuu uwe HALALI au “effective”  ni LAZIMA 2/3 (thelusi mbili) ya wanachama wawepo kwaajili ya huo mkutano ili uwe HALALI. Kwa record tulizo nazo, tunawanachama 586 hata kama walio jitokeza kupiga kura ni 400’s (mia nne na kitu) nikiangalia humu ndani tupo chini ya 2/3 ya wanachama hai (mkutano ulihudhuriwa na watu 28).  Sasa basi, swali langu la pili; kama huu ni mkutano mkuu, Je, tunacho kifanya hapa ni “constitutional” or “unconstitutional”. Akamaliza kwa kusema ana swali la tatu lakini angeomba ajibiwe hayo mawili. UKUMBI UKALIPUKA KWA MAKOFI.
Baada ya maswali hayo Ndg. Idd Sandaly alisimama na kukataa kujibu maswali hayo na kusema yatajibiwa mwisho. Solomn akasimama tena na kusema kuwa; maswali yangu ni msingi wa hiki kikao, akimaanisha kama hatuna 2/3 ya wanachama hai huu mkutano ni batili na uvunjwe. Wakati huo huo vijana wanao jiita Nyarugusu (Idd Green Guard) walianza kumvamia Dotto Malongo na kumwambia alicho kifuata atakipata. Vijana hao walikuwa ni Ally Musa, Abdi Makeo, Mussa Linga na Muddy Mabenzi "it was ignorance at its best".   Huku jamaa wanao jiita Nyarugusu wakienedelea kutaka kumpiga Dotto na Solom, Idd Sandaly alisimama na kusema yeye ndio anaongoza kikao na kikao kitaendelea. Ukweli ni kuwa hadi hapo kikao kilikuwa batili kwa kukosa 2/3 ya wanachama hai ambao ni wanachama 586. Ili kikao hiki kiwe HALALI kilihitaji mahudhurio ya wanachama 390 au 66% ya wanachama hai 586.
Baada ya maswali ya Solomon kukosa majibu huku vijana wanao jiita Nyarugusu (Idd Green Guard) wakitunisha misuli kama karume kenge; watu walitoka ukumbini na kikao kusimama kwa zaidi ya nusu saa. Saidi Mwamende aliita polis.  Polis walikuja na kuwaita Solomon, Dotto na Libe nje.  Polis waliwaeleza Solomon, Libe na Dotto kuwa “mtu aliye kodi huu ukumbi hataki nyinyi muwepo hapa, kwa hiyo ondokeni tu”. Solomn, Libe na Dotto walitii amri ya polis na kuondoka.

Video za matukio yote haya zipo na kwa sasa tunatoa mbili; moja Solomon akiuliza maswali na ya pili jamaa wanao jiita Nyarugusu (Ally Musa, Abdi Makeo, Mussa Linga na Muddy Mabenzi) walivyo taka kumvamia Dotto. Video zingine zinaonyesha jinsi Ally Mussa alivyo taka kumshambulia Solomon  na Saidi Mwamende alivyo taka kumvamia Solomon kwa sababu ameuliza maswali tu.   Hii ndio democrasia inayo letwa na uongozi huu BATILI. Video zote zipo zitatolewa muda muafaka ukifika.
Zaidi, tunayo video ya aliyekuwa katibu wa tume ya uchaguzi, Asha Nyang’anyi, akisema kuwa wanachama walio kuja hapa ndio wamelipia ada ya mwaka mziam$120.00 wengine wote ambao hawajaja walilipia mwezi mmoja $25.00, akimaanisha kuwa “quorum” imetimia na hao wengine ambao hawakuja sio hai.  Comment hii ya Asha nyang’anyi inasikitisha sana kwa kuona mtu aliye pewa dhamana ya kusimamia uchaguzi haijui katiba (ignorance of ATC constitution).  Katiba inazungumza wazi kuwa; mwanachama atakuwa hai kwa miezi mitatu zaidi hata kama hajalipa ada yake. Ikumbukwe kuwa, uchaguzi umefanyika mwezi uliopita. Hii inamaanisha hata wale wanachama walio lipia mwezi moja yaani wa nane; bado ni wanachama hai kwa miezi mitatu ijao hadi mwezi wa kumi na mbili.  Kauli ya Asha Nyang’anyi inaonyesha ni vipi uongozi huu ulivyo kuwa tayari kuwapoteza wanachama 586 baada ya miezi mitatu; kwani mahudhurio ya kwenye mkutano huu yalikuwa ya kukatisha tama. Ni watu 28 tu walio hudhuria.
MCHANGANUO ZAIDI WA MAHUDHURIO
Wanachama hai 586, Waliopiga kura 430, waliohudhuria kikao 28, mahudhurio haya yanakifanya kikao hiki kuwa batili kikatiba na hakina mamlaka yeyote ya kujadili katiba; Ukitoa watu wa Baord of Trustee waliofika kwenye mkutano ni 4; unapata mahudhurio ya watu 24; ukitoa wale viongozi ambao ni BATILI 4; unapata mahudhurio ya watu 20; ukitoa wale walio itiwa polisi bila hatia 3; unapata mahudhurio ya watu 17, ukiwatoa wanao jiita Nyarugusu (Idd Green Guard) walio kuja kuleta fujo 4; unapata mahudhurio ya watu 13. Kwa maana hii, mahudhurio halali ya mkutano huu mkuu ambao ni batili ulikuwa ni watu 13.
Chanzo: Swahilivilla

No comments :

Post a Comment