Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa hafla ya chakula cha usiku kilichoandiliwa na Kampuni ya Montage, ili kuchangia Watoto wa SOS Childrens Village Tanzania, kilichofanyika katika viwanja vya hoteli ya Serena Inn Zanzibar na kuwashirikisha Wafanyabiashara na makampuni ya Umma Tanzania.
Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni Utalii na Michezo Mhe. Bihindi Hamad, akizungumza wakati wa hafla hiyo na kumkaribisha Makamu wa Rais wa Tanzania Dk Bilal.
Mkurugenzi Mkuu wa SOS Childrens Village Tanzania Ndg. Anatori Rugaimukamu, akitowa maelezo wakati wa hafla hiyo ya chakula cha usiku kuchangia Watoto wa SOS na wenye mazingira magumu Tanzania, hafla hiyo imeandaliwa kwa pamoja na kampuni ya Montage na SOS, iliofanyika katika viwanja vya hoteli ya Serena Inn Zanzibar.
Baadhi ya Wananchi walioshiriki katika chakula cha usiku kuchangia watoto wa SOS kilichofanyika katika viwanja vya hoteli ya serena inn Zanzibar.
Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini wa Kijiji cha SOS Zanzibar wakifuatilia hafla hiyo maalum ilioandiliwa kwa ajili ya kuchangia watoto wa SOS na wenye mazingira magumu. wakimsikiliza Makamu wa Rais Dk Bilal akihutubia katika hafla hiyo iliofanyika katika viwanja vya hoteli ya serena inn Zanzibar.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Montage Tanzania Bi Teddy Mapunda akizungumza katika hafla hiyo na kutoa maelezo ya malengo ya Chakula hicho cha usiku kwa Wafanyabiashara waliohudhuria hafla hiyo na kutowa malengo kiasi cha fedha zinazohitajika kutokana na michango hiyo kiasi cha milioni mia mbili kusaidia watoto wa SOS na wanaoishi katika mazingira magumu. Hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya hoteli ya Serena Inn Zanzibar.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya SOS Zanzibar Bwa. Mohammed Baloo, akizungumza katika hafla hiyo ya kuchangisha fedha kwa ajili ya watoto wa SOS na wenye mazingira magumu.
Mtoto Mgeni Ali Ameir, shuhuda aliyelelewa katika Kijiji cha SOS mombasa Zanzibar akitowa maelezo katika hafla ya chakula cha usiku ili kuwachangia watoto wa SOS, jinsi alivyopata maelezo hadi kupata elimu ya Juu katika vyuo vikuu ndani ya tanzania na nje ya nchi kwa sasa ni Ofisa katika jumuiya ya kijamii akitumia elimu yake. aliyoipata kupitia SOS. kwa sasa ni mama wa familia.
Wafanyakazi wa SOS Childrens Village Tanzania wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal, wakati wa hafla ya chakula cha usiku kilichofanyika katika viwanja vya hoteli ya serena inn Zanzibar.
Makamu wa Rais wa Tanzania Dk. Mohammed Ghari Bilal akipokea mfano wa cheki kutoka kwa Meneja wa Hoteli ya Serena Inn Zanzibar ikiwa ni mchango wao kuwachangia Watoto SOS Childrens Village Tanzania, wakatika wa hafla ya chakula cha usiku kuchangia watoto hao.
Makamu wa Rais wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal akiungana na Wafanyabiashara katika hafla ya chakula cha usiku kilichoandaliwa na Kampuni ya Montage na SOS kwa ajili ya kuchangia Watoto wa SOS na walioko katika mazingira magumu, hala hiyo imefanyika katika viwanja vya hoteli ya Serena Inn Zanzibar.
Maofisa wa ZSSF wakiwa jkatika hafla ya chakula cha usiku kilichoandaliwa kwa ajili ya kuchangia Kijiji cha SOS kwa Watoto walioko katika mazingira magumu.
Wananchi na Wafanyabiashara walioshiriki katika hafla ya chakula cha usiku kuchangia Watoto wa SOS kilichoandaliwa na SOS na Kampuni ya Montage katika viwanja vya hoteli ya Serena Inn Zanzibar.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Montage Bi Teddy Mapunda akinadisha picha ya Makamu wa Rais Tanzania Dk Bilal iliochorwa na Watoto wa SOS wakatika wa hafla ya kuchangia iliofanyika katika viwanja vya hoteli ya Serena Inn Zanzibar. Picha hiyo imeuzwa kwa shilingi milioni mbili, katika mnada huo.
Makamu wa Rais wa Tanzania Dk. Mahomed Gharib Bilal akimkabidhi picha ya kuchora ya Makamu Rais wa Tanzania Dk. Bilal iliochorwa na Watoto wa SOS, Baada ya kununuliwa na Kampuni ya Turky kwa thamani ya shilingi milioni mbili akipokea Mkurugenzi wa Kampuni za Turky Tofik Salim Turky, wakati wa hafla ya chakula cha usiku kuchangia watoto wa Kijiji cha SOS.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Montage Bi Teddy Mapunda akinadisha picha ya Rais wa Zanzibar Dk Shein, iliochorwa na Watoto wa SOS wakatika wa hafla ya kuchangia iliofanyika katika viwanja vya hoteli ya Serena Inn Zanzibar. Picha hiyo imeuzwa kwa shilingi milioni moja na laki tatu katika mnada huo.
Makamu wa Rais wa Tanzania Dk. Mahomed Gharib Bilal akimkabidhi picha ya kuchora ya Rais wa Zanzibar Dk. Shein, iliochorwa na Watoto wa SOS, baada ya kununuliwa na PBZ kwa thamani ya shilingi milioni moja na laki tatu, akipokea picha hiyo Kaimu Mkurugenzi Masoko wa PBZ Seif Suleiman, wakati wa hafla ya chakula cha usiku kuchangia watoto wa Kijiji cha SOS.
Makamu wa Rais wa Tanzania Dk. Mohamed Gharib Bilal akimkabidhi Cheti Afisa wa Bank Kuu ya Tanzania Tawi la Zanzibar Ndg.Nicodemis K. Mboje, kwa mchango wao kuchangia Watoto wa SOS Children's Villages Tanzania. katika hafla hiyo zaidi ya Shilingi milioni miambili na laki tisa zimepatikana. kutokana na michango ya chakula cha ushiku zilizofanyika ili kukidhi mahitaji ya SOS.
Makamu wa Rais wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal akimkabididhi Cheti mwakilishi wa Kampuni ya Ndege ya PricesionAir, kwa mchango wao kuchangia Kijiji cha Watoto SOS na Watoto walioko katika mazingira magumu Tanzania. Wakati wa Chakula cha usiku kilichoandaliwa na SOSO NA Montage katika viwanja vya hoteli ya Serena Zanzibar.
Watoto wa Kijiji cha SOS Zanzibar wakicheza ngoma ya Kibati wakati wa Chakula cha Usiku kilichoandaliwa na Uongozi wa SOS na Montage kilichofanyika katika viwanja vya hoteli ya Serena Inn Zanzibar.
Chanzo: ZanziNews
No comments :
Post a Comment