
Wanasayansi wa Brazil na Ujerumani wanatumai kuutumia mnara huu katika uchunguzi wao wa vyanzo vya gesi chafu na mabadiliko ya hali ya anga.
Kutokana urefu wake, mnara huu utawezesha wanasayansi kuelewa mabadiliko ya mwelekeo wa upepo kwa kitalifa cha zaidi ya kilomita mia moja katika msitu wa Amazon. Msitu wa Amazon umekuwa ukikatwa kwa muda. Msitu wa Amazon ni kati ya misitu mikubwa zaidi duniani inayoathiri mazingira kwani inahusika pakubwa katika kuongeza na kupunguza kiwango cha hewa aina ya (carbon) angani.
Kulingana na bw. Paulo Artaxo, mwelekezi wa mradi huo kutoka chuo kikuu cha Sao Paulo, amesema mnara huo utasaidia pakubwa katika juhudi za kutafuta majibu ya maswali mengi kuhusu mabadiliko ya hali ya anga duniani. Aidha, mnara huu unatarajiwa kutumiwa pamoja na minara mingine midogo ambayo tayari imejengwa nchini humo. Kulingana na wajenzi, mnara huu utafanana na ule uliojengwa Siberia ya kati katika mwaka wa 2006.
Chanzo: Mtayarisho blog
No comments :
Post a Comment