Waziri wa Fedha Omar Yussuf Mzee akizungumza na ujumbe wa Wafanyabiashara wa Makamupuni ya uwekezaji kutoka Ubelgiji walipomtembelea Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Balozi wa Tanzania Nchini Ubelgiji Dkt. Diodorus B. Kamala akielezea lengo la ujio wa wawekezaji kutoka Ubelgiji kuja kuwekeza nchini Tanzania alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kufuatia ujio wa wawekezaji wa nchi hiyo Zanzibar.
Waziri wa Fedha Zanzibar Mhe. Omar Yussuf Mzee akiwa katika picha ya pamoja na Wawekezaji kutoka Ubelgiji kuja kuwekeza Tanzania, wakiwa nje ya jengo la Wizara ya Fedha Vuga Zanzibar baada ya mazungumzo yao na Waziri.wa Fedha Zanzibar.
Waziri wa Miundombinu na Mawasilino Juma Duni Haji akiwa na watendaji wake wakuu wakimsikiliza Meneja mauzo wa Kampuni ya ujenzi ya Anglo Belgian Corporation ya Ubelgiji walipofanya mazungumzo Ofisini kwake Kisauni.
Wamiliki wa makampuni toka Ubelgiji wakimsikiliza Mkurugenzi Uenezi wa Mamlaka ya Uendelezaji Vitega Uchumi Zanzibar (ZIPA) Bi. Nasria Mohd Nassor (hayupo pichani) walipofika ofisini kwake Maruhubi Mjini Zanzibar.
Afisa Mipango wa Shirika la Bandari Zanzibar Ali Haji akizungumza na wamiliki wa makampuni kutoka Ubelgiji walipotembelea bandari ya Malindi mjini Zanzibar.
Chanzo: ZanziNews
No comments :
Post a Comment