Mkurugenzi Mkuu wa Chuo cha Zanzibar Education College Ndg. Ussi Said Suleiman akizungumza na kutowa mafanikio ya Chuo Chao kwa Mgeni rasmin wakati wa Mahafali ya Tatu ya Chuo hicho tangu kuazishwa kwake kutowa Elimu kwa Vijana kwa ajili ya Skuli za Maandalizi na lugha ya Kiingereza.
Mwakilishi Jimbo la Kiwani Pemba Mhe. Hija Hassan Hija,akitowa nasaha zake kwa Wahitimu wa Chuo cha Zanzibar Education College, wakati wa mahafali ya tatu ya Chuo hicho na kuwataka kuitumia vizuri elimu walioipata kwa walengwa wanapokuwa katika kazi zao ya ufundishaji na kuahidi kutowa msaada wa shilingi laki mbili kusaidia kupata eneo lao kutolea Elimu kwa Vijana wa Kizanzibar wanaojiunga na chuo hicho.
Mkurugenzi wa Idara ya Vijana Zanzibar Ndg. Mohammed Salum, akitowa nasaha zake kwa Vijana wahitimu wa Chuo cha Zanzibar Education College, na kuwataka kutowa Elimu wanayoipata kama Walivyofundishwa chuoni kwa Watoto wac Skuli za Maandalizi Zanzibar.
Wahitimu wa Mahafali ya Tatu ya ZEC.
Wazazi na Walezi wa watoto wanaosoma katika Skuli ya VIP na Chuo cha Zanzibar Education College wakifuatilia mahafali hayo.
Wazazi na Walezi wa watoto wanaosoma katika Skuli ya VIP na Chuo cha Zanzibar Education College wakifuatilia mahafali hayo.
Mkalimani wa lugha za alama akitowa muongozi kwa Watu wenye ulemavu wa kutokusikia wakati wa mahafali hayo katika viwanja vya chuo hicho mwanakwerekwe Zanzibar.
Waheshimiwa Marais wa Nchi mbalimbali walioalikwa katika Mahafali ya Tatu ya Chuo cha Zanzibar Education College wakifuatilia hafla ya sherehe hiyo katika viwanja vya Chuo cha ZEC Mwanakwerekwe Zanzibar.
Mkurugenzi wa Idara ya Vijana Zanzibar Ndg Mohammed Salum, akimkabidhi Cheti chake Mhitimu wa Chuo cha Zanzibar Education College baada ya kumaliza Mafunzo yake Chuoni hapo.
Wahitimu wa Mafunzo ya Ualimu wa Skuli za Maandalizi Chekechea, wakiangalia vyeti vyao baada ya kukabidhiwa wakati wa mahafali yao Tatu ya Chuo hicho yaliofanyika katika viwanja vya Chuo hicho Mwanakwerekwe Zanzibar.
Wahitimu wa Chuo cha Zanzibar Education College wakisoma ngonjera katika hafla hiyo ya mahafali ya Tatu ya Chuo chao yaliofanyika katika viwanja vya Chuo hicho Mwanakwerekwe Zanzibar.
Mwanafunzi wa Chuo cha ZEC akiekti kama Rais Obama akiwa ni mmoja wa mualikwa katika mahafali hayo ya Chuo cha ZEC.akihutubia wakati wa sherehe hizo.
Rais wa Burundi akihutubia katika mahafali ya tatu ya Chuo cha ZEC, akiwa mgeni mualikwa katika mahafali hayo.
Mwanafunzi wa Chuo cha Zanzibar Education College akiwa katika igizo la Rais wa Sudan, akiwa mualikwa katika mahafali hayo.ya Tatu ya Chuo cha ZEC. Zanzibar.
Wanafunzi wa Chuo cha Zanzibar Education College. wakitowa nadharia ya kujifunza lugha ya kiingereza wakati wa hafla ya mahafali ya tatu ya chuo hicho yaliofanyika katika viwanja vya Chuo hicho Mwakwerekwe Zanzibar. Hutoa Mafunzo ya lugha ya Kiingereza na nyeginezo kwa Wanafunzo wanaojiunga na Chuo hicho.
Wanafunzi wa Skuli ya VIP,wakicheza ngoma wakati wa hafla ya Mahafali ya Tatu ya Chuo cha ZEC, Kinachotowa mafunzo kwa Walimu wa Skuli za Chekechea (Maandalizi).
Wanafunzi wa Maandalizi wa Skuli ya VIP, wakifuatilia sherehe za Mahafali ya Chuo chao katika viwanja vya Skuli hiyo Kwerekwe Zanzibar.
Mgeni rasmin akifuatilia michezo wakati wa mahafali ya tatu ya Chuo cha ZEC Mwanakwerekwe Zanzibar.
Wanafunzi wa ZEC wakishangilia wakati wa hafla ya Chuo chao yaliofanyika katika viwanja vya Chuo hicho.
Mkurugenzi wa Idara ya Vijana Zanzibar Ndg Mohammed Salum na Mwakilishi Jimbo la Kiwani Pemba Mhe. Hija Hassan Hija, na Mkurugenzi Mkuu wa Chuo cha Zanzibar Education College Ndg Ussi Said Suleiman, wakiwa katika picha ya pamoja na wahitimu wa Chuo hicho wakati wa sherehe za Mahafali ya Tatu ya Chuo hicho yaliofanyika katika viwanja vya chuo hicho Mwanakwerekwe Zanzibar.
Chanzo: ZanziNews
No comments :
Post a Comment