Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, December 18, 2014

Profesa Tibaijuka: sina hatia, siwezi kujiuzulu

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka 
Na Peter Edson

KWA UFUPI
Akizungumza na waandishi wa habari asubuhi jijini Dar es Salaam, Profesa Tibaijuka amesema kuwa pamoja na kuwepo kwa shinikizo la kutaka kujiuzuru, yeye binafsi ameona hana sababu ya kufanya hivyo kwani kufanya hivyo ni kukubali kuwa amehusika moja kwa moja kwenye kashfa hiyo jambo ambalo si la kweli.
Siku Moja baada ya kujiuzuri kwa Mwanasheria mkuu Jaji Fredrick Werema, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka kwa mara nyingine amejitokeza hadharani na kutoa msimamo wake kwamba hana sababu ya kujiuzuru kwenye nafasi yake kwa kuwa hakuhusika kwa namna yeyote kwenye sakata la uchotwaji wa mabilioni kwenye akaunti ya Escrow.
Akizungumza na waandishi wa habari asubuhi jijini Dar es Salaam, Profesa Tibaijuka amesema kuwa pamoja na kuwepo kwa shinikizo la kutaka kujiuzuru, yeye binafsi ameona hana sababu ya kufanya hivyo kwani kufanya hivyo ni kukubali kuwa amehusika moja kwa moja kwenye kashfa hiyo jambo ambalo si la kweli.
Profesa Tibaijuka amekwenda mbali zaidi na kusema kuwa uvumi unaoendelea kusambazwa mitaani ni ishara mbaya kwani unawaaminisha wananchi kuwa amehusika katika sakata hilo wakati yeye hajahusika na jambo lolote.
“Huu uvumi unatakiwa kuachwa, sioni sababu yeyote ya mimi  kujiuzuru kwa kuwa sijahusika kwa namna yeyote kwenye sakata hili la Escrow” anasema Profesa Anna Tibaijuka.
http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Profesa-Tibaijuka--sina-hatia--siwezi-kujiuzuru/-/1597296/2561046/-/hwx78d/-/index.html
Join the discussion…

  • Avatar


    Mama haelewi hata kama hukuchukua na mali ya wizi ikakutwa kwako na wewe unaonekana unaushirika na mwizi. Kwa kuwa hukuhusika na fedha imeonekana ni ya wizi ushauri wangu kwako ni kurudisha fedha hiyo, pili omba radhi watanzania kwa kuwa huwezi kisema hukushiriki na fedha hizo bado unazitumia..acha kutufanya mazuzu, tumeamka na ukweli naona unaukataa wazi ingawa moyoni mwako unajua. Hutazikwa na chochote marabuondokapo hapa duniani, rejesha fedha hiyo ya maskini...wako ndugu zako wengi wanalala kwenye ngozi na watoto wengi wanaokaa chini na kutembea bila viatu...ona aibu basi


      • Avatar


        Mmmh!!! sasa ni wazi kwa nini Rais Kikwete ana kigugumizi cha kuwachukulia hatua waliokwapua fedha za ESCROW...sijui ile ahadi ya mwana-TANU (na baadaye ikarithishwa kwa CCM) inayosema ..."Rushwa ni adui wa haki, sitatoa wala kupokea rushwa" nayo imewekwa kwenye freezer kama walivyofanya kwa "Azimio la Arusha"? sijui tunakwenda wapi!!


          • Avatar


            Huyu mama naona ingawa ni msomi haelewi maana ya uwajibikaji .Yeye kama waziri na msimamizi mkuu wa wizara yake na uamuzi wowote utolewayo na wizara yake ,yeye ndiye muhusika mkuu,hivyo kama wizara imeboronga na yeye kama kiongozi mtendaji mkuu anapaswa kuwajibishwa.Ina maana atafukuzwa kazi na afunguliwe mashitaka,kama mh. rais akishindwa kumwajibisha ,basi rais ajaye 2015 aanze kuwawajiobisha hawa walio ktk scandal ya ESCROW!!

          No comments :

          Post a Comment