Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, December 11, 2014

Zitto apeleka moto wa kufichua ufisadi kwa wawakilishi ZANZIBAR!

“Kwa hiyo ni wajibu wa PAC kuhakikisha kuwa Taarifa ya CAG inafikishwa Barazani, inajadiliwa na kuamuliwa.” Zitto 
Na Mwandishi Wetu, Mwananchi
Kwa ufupi
“Ni muhimu kuzingatia kwamba wawakilishi ndiyo chombo cha mwisho katika uamuzi kuhusu masuala ya wananchi wa Zanzibar ikiwamo matumizi ya fedha za umma.”

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe amewataka wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wanaounda kamati hiyo, kufanya kazi kama ilivyo kamati yake kwa Tanzania Bara.

Zitto aliyasema hayo jana kwenye semina ya wawakilishi hao iliyofanyika jijini hapa ambapo alisema, kamati husimamia matumizi yote ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliyoidhinishwa na baraza na kutoa taarifa zake kwa Umma.

Alisema hesabu za Serikali huendana na Ripoti ya CAG ambayo ndiyo nyenzo kuu ya Baraza katika kusimamia fedha za umma.

Hata hivyo, Zitto alisema PAC inapoona inafaa, huagiza ukaguzi maalumu kwenye maeneo mahususi na njia hiyo imesaidia kuibuliwa kwa mambo mengi ya ufisadi wa fedha za umma kwa Tanzania Bara.
“Kuna nyakati mkaguzi anakuwa haoni masuala fulani hadi anapoombwa na vyombo vingine na hata wananchi…Ni vyema Kamati ya PAC Zanzibar kutumia pia njia hii ili kuimarisha usimamizi bora wa fedha za umma kwa Zanzibar kama ilivyo sasa katika Jamhuri ya Muungano,” alisema Zitto na kuongeza;

“Ni muhimu kuzingatia kwamba wawakilishi ndiyo chombo cha mwisho katika uamuzi kuhusu masuala ya wananchi wa Zanzibar ikiwamo matumizi ya fedha za umma.”

Ni muhimu kuhakikisha kuwa Wizara ya Fedha ya Zanzibar inajibu hoja za PAC (treasury notes) na hapo ndipo mzunguko wa uwajibikaji unakuwa umekamilika.

Alisema ni wakati wa kufikiria namna ambavyo CAG na PAC wanaweza kutimiza wajibu wao katika kuzuia matumizi yanayoelekea kutokuwa na ufanisi.

http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Zitto-apeleka-moto-wa-kufichua-ufisadi-kwa-wawakilishi-Z-bar/-/1597296/2552210/-/hgcely/-/index.html

No comments :

Post a Comment