zanglassworks

AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, February 28, 2015

Kikundi cha ‘Tano ladies’ cha wanawake Watanzania waishio Jiji la Washington DC, Marekani, watoa mashine ya kupima saratani Lugalo.

Salma Kikwete akabidhi mashine ya kupima saratani Lugalo.

28th February 2015
Mke wa Rais, Salma Kikwete akikabidhi mashine ya kupimia saratani ya matiti katika hospitali ya Lugalo kwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi Luteni Jenerali Samuel Ndomba katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika katika Hospitali hiyo jijini Dar es Salaam jana.

Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), imekabidhi mashine ya kupimia ugonjwa wa saratani ya matiti yenye thamani ya dola za kimarekani 200,000 kwa hospitali ya Lugalo, jijini Dar es Salaam.
 
Mke wa Rais, Salma Kikwete, alikabidhi msaada huo jana uliotolewa na kikundi cha ‘Tano ladies’ cha wanawake Watanzania waishio Jiji la Washington DC, Marekani.
 
Kikundi hichi kinaundwa na wanawake wataalamu wenye taaluma tofauti wakiwamo wana-Sayansi na kimejikita kurudisha maendeleo Tanzania.
 
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kupitia ubalozi wake Washington DC umekuwa ukiwahamasisha Watanzania waishio ugaibuni kuwekeza nchini ambapo moja ya michango iliyotolewa na watu hao ni mashine hiyo waliyomkabidhi mama Salma, Septemba mwaka jana. Mama Salma alisema saratani ya matiti inaongoza ikifuatiwa na shingo ya kizazi wakati kwa upande wa akina baba husumbuliwa na tezi dume.
 
Alitoa wito kwa wanawake kujitokeza kupima maradhi hayo ambayo kama hayajagundulika mapema husababisha kifo.
 
“Nakishukuru kikundi hichi cha wanawake wamarekani kwa kutambua afya ya mama, mashine hizi zinahitajika na wajibu wetu tuzipatapo tuzitunze zitufae sisi na kizazi kijacho, naomba ianze kazi mara moja,” alisema.
 
Alisema wametoa msaada huo kwenye hospitali hiyo kwa sababu wamekuwa wakitoa huduma ya mama na mtoto pamoja na asilimia 80 ya wanaotibiwa hapo kuwa ni raia wa kawaida.
 
“Wataalam wanasema kupima saratani ni mara moja baada ya miaka mitatu, Watanzania tutumie fursa hii kupima afya zetu, saratani ya shingo ya kizazi, matiti na tezi dume zinatibika ikiwa tu tutawahi mapema,” alisema.
 
“Saratani huwakosesha wanawake matumaini kwa sababu wao ni mama na unakuta wanamajukumu makubwa kwenye familia ya kulea watoto, lakini nisiwakatishe tamaa ‘kina mama mnapoona mvua zinanyesha wakati wa kiangazi ujue kuna tatizo hapo na hayo ni mabadiliko ya tabia nchi jitokezeni kupima saratani’ msikae kimya,” alisema.
 
Pia aliwahamasisha wanaume hasa wenye umri wa miaka 45 kujitokeza kupima saratani ya tezi dume ambayo ni tishio la maisha yao.
 
Mnadhimu Mkuu wa jeshi hilo, Luteni Jenerali Samwel Ndomba, aliishukuru Wama kwa msaada huo na kueleza kuwa, utasaidia kutoa huduma siyo tu kwa wanajeshi na familia zao bali pia, wananchi wanaofika hapo kutibiwa.
 
Alisema kuwa kujua hali ya afya mapema husaidia kupanga maisha ya baadae.
 
Naye, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda, aliishukuru Wama kwa kuona umuhimu na kugusa afya za kina mama ambao ni moja ya chachu ya maendeleo ya Taifa.
 
Alisema kupitia mashine hiyo anaamini saratani ya matiti  sasa itapungua kwa sababu watu watapima mapema afya zao na kupata matibabu.
 
Naibu Katibu Mkuu kutoka Wizara ya Ulinzi wa Kujenga Taifa, Rose Shelukindo, alisema kuwa mashine hiyo ni mkombozi wa afya za wanawake.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment