Kadhi Mkuu wa Zanzibar Shekh. Khamisi Haji Khamis akiongoza Sala ya kuusalia mwili wa marehemu Salmin Awadh Salmin, katika masjid Muhammad Mombasa kwa Mchina, katika Sala hiyo amehudhuria Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK Ali Mohamed Shein, Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Mohammed Gharib Bilal, Rais Mstaaf wa Zanzibar Dk. Amani Karume, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, na Viongozi mbalimbali wa Vyama vya Siasa Tanzania.
Dk Shein Awafariji Wanafamilia ya Marehemu Salmin Awadh Alipofika Nyumbani kwao Magomeni.
Rais wa Zanzibar na Mwenmyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai alipofika kutoa pole Nyumbani kwa Marehemu Salmin Awadhaliyekuwa mwakilishi wa Jimbo la Magomeni (CCM)Magomeni Mjini Unguja leo
Rais wa Zanzibar na Mwenmyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (wa tatu kushoto) pamoja na Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi na Viongozi wengine walipofika kutoa pole kwa wafiwaNyumbani kwa Marehemu Salmin Awadh aliyekuwa mwakilishi wa Jimbo la Magomeni (CCM) Magomeni Mjini Unguja leo
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein na Waziri wa Uwezeshaji,Ustawi wa Jamii,Vijana,Wanawaker na Watoto Bi Zainab Omar Mohamed (katikati) pamoja na wake wa Makamo wa Pili wa Rais na Kinamama wakijumuika kwa pamoja katika maziko ya Marehemu Salmin Awadh aliyekuwa mwakilishi wa Jimbo la Magomeni (CCM) nyumbani kwake Magomeni Mjini Unguja leo
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein alipofika kutoa pole kwa kizuka wa Marehemu Salmin Awadh aliyekuwa mwakilishi wa Jimbo la Magomeni (CCM) nyumbani kwake Magomeni Mjini Unguja leo
Wananchi kutoka sehemu mbali mbali kike kwa kiume walijumuika pamoja katika maziko ya Marehemu Salmin Awadh aliyekuwa mwakilishi wa Jimbo la Magomeni (CCM) nyumbani kwake Magomeni Mjini Unguja leo na kuzikwa kijijini kwao Makunduchi Wilaya ya Kusini Unguja,[Picha na Ikulu.],
[Picha na Ikulu.]
Mwili wa Marehemu Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni Salmin Awadh Salmin Ukumbi wa Baraza Chukwani Zanzibar.
Mwili wa marehemu Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni Salmin Awadh Salmin ukiwa mbele ya ukumbi wa Baraza kwa ajili ya kutowa heshima za mwisho na kuuaga kwa Wananchi na Wajumbe waliofika katika ukumbi huo Chukwani Zanzibar.
Waheshimiwa Wabunge na Wawakilishi na Wananchi wakishiriki katika dua ya kuuaga mwili wa marehemu Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi na Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni Zanzibar Salmin Awadh Salmin. aliyefariki hafla jana 19-2-2015 baada ya kuugua hafla akiwa katika kazi zake za kawauidi Afisi Kuu ya CCM Zanzibar.
Shekh Noman Thabit Jongo akitowa mawaidha wakati wa kuuaga mwili wa marehemu iliofanyika katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakifuatilia mawaidha yakitolewa na Shekh Naman Thabit Jongo, akitowa nasaha za dini kwa wananchi waliohudhuria katika kuuaga mwili wa marehemu iliofanyika katika ukumbi wa baraza.
Waheshimiwa wakiwa na majonzi wakifuatilia mawaidha yaliokuwa yakitolewa.
Wajumbe wakiwa na simazi ya kuondokewa na Mwakilishi mwezao wa Jimbo la Magomeni Salmin Awadh Salmin, kilichotokea hafla jana mchana.
Naibu Waziri wa Fedha Tanzania Mhe Malima wakiwa katika ukumbi wa Baraza akifuatilia mawaidha yaliokuwa yakitolewa wakati wa kuuaga mwili wa marehemu Salmin Awadh Salmin.
Wawakilishi wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakiwa na majonzi ya kufiwa na mmoja wa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni Zanzibar Salmin Awadh Salmin, wakisikiliza mawaidha yaliokuwa yakitolewa na Shekh Noman Thabit Jongo.
Wafanyakazi wa Baraza la Wawakilishi wakishiriki katika kuuaga mwili wa marehemu Salmin Awadh Salmin iliofanyika katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani.
Kadhi Mkuu wa Zanzibar Shekh. Khamis Haji Khamis akisoma dua kumuombea marehemu Salmin Awadh Salmin iliofanyika katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad , akijumuika na Wawakilishi na Wabunge katika hafla ya kuuaga mwili wa marehemu Salmin Awadh Salmin iliofanyika katika ukumbi wa baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Waheshimiwa Wabunge na Wawakilishi wakijumuiya katika dua ya pamoja ya kuuombea mwili wa marehemu Salmin Awadh Salmin, iliofanyika katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi.
Wawakilishi wakijumuika katika dua iliokuwa ikisomwa na Kadhi Mkuu wa Zanzibar Shekh Khamis Haji Khamis.
Waheshimiwa Wawakilishi wakiwa na majonzi ya kuondokewa na Mwakilishi mwezao hafla jana wakiwa katika maombolezi katika ukumbi wa Baraza ulipoletwa kuuagwa na Wajumbe na Wananchi wengini ukumbini hapo.
Waheshimiwa Wabunge na Wawakilishi wakihudhuria hafla ya kuuaga mwili wa Marehemu Salmin Awadh Salmin ulipofikishwa katika ukumbi wa baraza Chukwani Zanzibar.
Askari wa Baraza la Wawakilishi wakiwa wameubeba mwili wa marehemu Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni Mhe Salmin Awadh Salmin,wakitoka katika ukumbi wa baraza baada ya kumaliza kutoa dua.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakitoka ukumbi wa Baraza baada ya kumalizika kwa dua maalum ya kumuaga aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni Mhe Salmin Awadh Salmin.
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakitowa ukumbi wa Baraza baada ya kumalizika kwa Dua ya kuuombea mwili wa marehemu Salmin Awadh Salmin, iliofanyika katika ukumbi huo kulia Mwakilishi wa Jangombe Mhe Suleiman Othman Nyanga , Mwakilishi wa Uzini Mhe Mohammed Raza na Mwakilishi wa Rahaleo Mhe Nassor Salim Jazira, wakitoka ukumbi wa baraza baada ya kumalizika kwa Dua maalum ya kumuaga marehemu.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akisalimaia na Waziri Mkuu Mstaaf wa Tanzania Mhe Edward Lowasa wakiwa katika viwanja vya Baraza la Wawakilishi walipohudhuria katika hafla ya kuuaga mwili wa marehemu na kusoma dua.
Shekh Noman Thabit Jongo akiongoza sala ya kumsalia marehemu Salmin Awadh Salmin aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni Zanzibar aliyefarika jana hafla akiwa katika kazi zake za Kichama Afisi Kuu Kisiwandui Zanzibar.
Wahesshimiwa Wajumbe wa Bdaraza la Wawakilishi Zanzibar wakiitikia dua baada ya kuusalima mwili wa marehemu Salmin Awadh Salmin katika Masjid Taqkua uliopo katika viwanja vya Baraza Chukwani. dua ilioongozwa na Shekh, Noman Thabit Jongo.
Wasifu wa Marehemu Salmin Awadh Salmin Aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni Zanzibar.
WASIFU WA MAREHEMU MHESHIMIWA SALMIN AWADH SALMIN, MWAKILISHI WA JIMBO LA MAGOMENI
Baraza la Wawakilishi Zanzibar, limepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa, kifo cha Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni Zanzibar, Mheshimiwa Salmin Awadh Salmin kilichotokea baada ya kuugua ghafla hapo jana Alkamis tarehe 19. 02. 2015 wakati akiwa katika kikao cha kikazi cha kichama. Mheshimiwa Salmin Awadh ambaye alikuwa Mwakilishi tangu Octoba 2005, alizaliwa tarehe 06. 06. 1958 huko Makunduchi, Wilaya ya Kusini, Mkoa wa Kusini Unguja.
Marehemu Salmin Awadh alipata elimu yake ya msingi katika Skuli ya Kiongoni kuanzia mwaka 1963 na baadaye kuendelea na masomo ya sekondari katika Skuli ya Sekondari ya Makunduchi. Vile vile Marehemu alijiunga na Chuo cha Uchumi Zanzibar mwaka 1971 hadi mwaka 1974.
Marehemu Mheshimiwa Salmin Awadh aliwahi kujiunga na kazi ya Ulinzi kupitia Jeshi la Wananchi JWTZ kuanzia 1976 hadi 1986 na kufikia cheo cha Sergent. Mbali ya kazi ya hiyo ya Ulinzi, Marehemu aliwahi kuwa Meneja katika Hoteli ya Narrow Street, Zanzibar baina ya mwaka 2000 na mwaka 2005.
Katika shughuli za kisiasa, marehemu amewahi kushika nyadhifa mbali mbali katika Chama cha Mapinduzi ikiwemo Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya tawi la Magomeni kuanzia mwaka 1982 hadi 1992, Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Jimbo la Magomeni tangu mwaka 1992. Mnamo mwaka 1995 hadi mwaka 2000 marehemu Salmin Awadh alikua Diwani wa Magomeni.
Mheshimiwa Salmin alikuwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi wa Jimbo la Magomeni, kupitia Chama cha Mapinduzi tangu Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005 na kuendelea na wadhifa huo hadi kufariki kwake. Aidha Marehemu alichaguliwa Kuongoza Kamati mbali mbali ikiwemo Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Fedha na Uchumi ya Baraza la Wawakilishi pamoja na Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo ya Baraza la Wawakilishi, Kamati ambayo alikuwa anaiongoza hadi kufariki kwake.
Vile vile kutokana na umakini wake na nidhamu ya utendaji kichama mnamo mwezi Juni, 2011 Marehemu alichaguliwa kuwa Mnadhimu wa Chama cha Mapinduzi ndani ya Baraza la Wawakilishi ambapo kwa nafasi hiyo alikuwa pia Mjumbe wa Halmashauri Kuu na Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi wadhifa ambao ameendelea nao hadi kufarika kwake.
Marehemu Salmin Awadh pia alikuwa miongoni mwa Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba na alitowa mchango mkubwa katika Bunge la Katiba ambapo alikuwa Makamo Mwenyekiti wa Kamati namba 10 ya Bunge hilo. Aidha kutokana na uelewa wake wa masuala mbali mbali Marehemu alichaguliwa kuwa Makamo Mwenyekiti wa Bodi ya Gazeti la Zanzibar leo tokea mwaka 2009 hadi kufariki kwake.
Katika kipindi chote cha kuwawakilisha wananchi wa Jimbo la Magomeni, Marehemu alikuwa mtetezi mkubwa wa maslahi ya wananchi wa jimbo hilo pamoja na wananchi wote wa Zanzibar na aliifanya kazi yake hiyo kwa moyo wake wote, uadilifu na mashirikiano makubwa na Wajumbe wenzake wa Baraza la Wawakilishi.
Ni dhahiri kuwa Baraza la Wawakilishi, Chama cha Mapinduzi, Wananchi wa Jimbo la Magomeni na wananchi wote kwa jumla, wameondokewa na mtu muhimu na mahiri mwenye kujiamini katika kusimamia anachokiamini katika kuleta maendeleo ya Taifa.
Marehemu ameacha kizuka na watoto saba.
Tunamuomba Mwenyezimungu aijaalie familia ya Marehemu pamoja na wananchi wa Jimbo la Magomeni, subira na utulivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba. Tukielewa kwamba sote ni waja wa Mwenyezi Mungu na hapana shaka marejeo yetu ni kwake.
Mwenyezi Mungu aiweke roho ya Marehemu mahali pema peponi. Amin.
Amour M. Amour
MKUU WA UTAWALA
BARAZA LA WAWAKILISHI
ZANZIBAR.
20 Februari, 2015.
No comments :
Post a Comment