Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Celina Kombani alipofika Ikulu Mjini Zanzibar akiongoza Ujumbe wa Bodi ya Udhamini wa Mfuko wa kuwaenzi Waasisi wa Taifa leo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Celina Kombani (aliyesimama) akisoma taarifa ya wajumbe wa Bodi ya Udhamini wa Mfuko wa kuwaenzi Waasisi wa Taifa wakati wajumbe walipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo asubuhi (wengine) Mwenyekiti Vikabenga Nsa Kaisi (wa pili kushoto) na Aisha Ali Karume Mjumbe (kushoto).
Miongoni mwa wajumbe wa Bodi ya Udhamini wa Mfuko wa kuwaenzi Waasisi wa Taifa walipofika kuzungumza na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein leo asubuhi katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar (kutoka kulia) Aisha Ali Karume na Asha Kombo Haji na Rase-Mary J.Nyerere, [Picha na Ikulu.]

Rais Shein Asema Serekali za SMZ na SMT Ziko Tayari Kushirikiana na Bodi ya Udhamini ya Mfuko wa Kuwaenzi Waasisi wa Taifa
STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Zanzibar 21.1. 2015
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa upande wake sambamba na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ziko tayari kushirikiana na Bodi ya Udhamini ya Mfuko wa Kuwaenzi Waasisi wa Taifa kutokana na mchango wao mkubwa kwa Taifa hili.
Dk. Shein aliyasema hayo leo huko Ikulu mjini Zanzibar wakati alipokutana na Wajumbe wa Bodi ya Udhamini wa Mfuko wa Kuwaenzi Waasisi wa Taifa ulioongozwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mhe. Celina Kombani.
Katika maelezo yake, Dk. Shein alisema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya uongozi wake na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya ungozi wa Dk. Jakaya Mrisho Kikwete wako tayari kulianza na kuliunga mkono jambo hilo ambalo lina umhumimu mkubwa kwa Taifa.
Alisema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itahakikisha inashiriki kikamilifu katika kushiriki na kufanikisha yale yote yatakayohitajika katika kuimarisha na kuendeleza Bodi hiyo.
Dk. Shein alisema kuwa nchi nyingi duniani zimekuwa na utamaduni wa kuwaenzi waasisi wao na kwa upande wa Tanzania ni bahati ilioje kuwa na waasisi ambao wameikomboa Zanzibar na Tanganyika na baadae kuifanya kuwa moja.

Pamoja na hayo, Dk. Shein aliwapongeza Wajumbe hao kwa kuanza kuitekeleza Sheria ya Kuwaenzi Waasisi wa Taifa ambayo wakati wa mchakato wake alishiriki kikamilifu akiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya uongozi wa Rais Mstaafu Benjamin Willium Mkapa.
Aidha, Dk. Shein alisema kuwa kuwepo kwa kituo cha Kuwaenzi Waasisi wa Tauifa ambachio kitatumika kuhifadhi vitu na kumbukumbu zao ili kudumisha historia na fikra zao kwa maslahi na urithi wa Taifa vitakuwa chachu katika kuwavutia watalii.
Mapema Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mhe. Celina Kombani alieleza kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutambua mchango mkubwa uliotolewa na Waasisi wa Taifa hili, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Sheikh Abeid Amani Karume iliamua kuanza juhudi za kuendeleza urithi wa kihistoria waliouacha Waasisi hao.
Alisema kuwa heshima, utu, amani na utulivu, demokrasia na maenddleo ya Mtanzania ni urithi na utajiri kwa Taifa hili ambao umetokana na juhudi, mchango mkubwa na kujitoa mhanga kwa viongozi hao, hivyo hakuna budi kuyalinda kwa kuwaenzi.
Alisisitiza kuwa moja kati ya juhudi kubwa za Serikali ni kutunga na kupitisha Sheria ya Kuwaenzi Waasisi wa Taifa hili namba 18 ya mwaka 2004.
Alisema kuwa Sheria hiyo pamoja na mambo mengineyo inawataka kuanzisha Kituo cha Kuwaenzi Waasisi wa Taifa ambacho kitatumika kuhifadhi vitu na kumbukumbu zao ili kudumisha historia na fikra zao kwa maslahi ya urithi wa Taifa.
Aidha, alisema kuwa Bodi hiyo ya Udhamini ya Mfuko huo ambayo imefika Ikulu kujitambulisha kwa Rais ina kazi nyingi ikiwa ni pamoja na kuratibu na kusiamamia uendeshaji wa Vituo vya Kuwaenzi Waasisi kwa misingi ya uwazi na usawa ili kuviwezesha vituo kufanya shughuli zake kwa kuzingatia maslahi ya Taifa.
Sambamba na hayo, Bodi hiyo ina kazi ya kusimamia na kuandaa programu mbali mbakli zinazohusukuwaenzi Waasisi zenye tija kwa Taifa mfano programu za elimu kwa umma, maadhimisho, maonyesho, mijadala na mabo mengineyo.
Waziri Kombani alisema kuwa Fedha zinazopatikana kutokana na Mfuko huo zinatumika kugharamia uendeshaji wa Vituo vya kuwaenzi Waasisi wa Taifa ikiwa ni pamoja na kujenga vituo katika pande zote mbili za Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania.
Nae Dk. John Magoti akitoa neno la shukurani alieleza kufarajika kwa Wajumbe wa Bodi hiyo kutokana na maelezo ya Dk. Shein kwa kuonesha kuwa tayari kwa Serikali zote mbili ile ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika kuiunga mkono Bodi hiyo ili ipate kufikia malengo iliyojiwekea.
Dk. Magoti alisema kuwa kwa niaba ya Wajumbe hao wa Bodi hiyo juhudi za makusudi watazichukua katika kuhakikisha mafanikio makubwa yanapatikana katika uongozi wao kwani hatua hiyo ina lengo kubwa la kuenzi historia ya waasisi wa Taifa hili.
Miongoni wa Wajumbe wa Bodi hiyo ni Mwenyekiti wa Bodi Kanali Mstaafu Kabenga Nsa Kaisi, Katibu wa Charles Magaya na Wajumbe ni Mama Fatuma Karume, Madaraka Julius Nyerere, Rosemary Julius Nyerere, Mwatumu Jasmine Malale, Dk. John Magoti, Asha Ali Karume, Asha Kombo Haji na Issa Ibrahim Mahmoud.
Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar
No comments :
Post a Comment