Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, March 27, 2015

CUF yataka kura ya maoni iahirishwe.


Naibu Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CUF, Abdul Kambaya

Shinikizo la kutaka upigaji wa kura ya maoni ya katiba inayopendekezwa uliopangwa kufanyika Aprili 30, mwaka huu, usitishwe, limezidi kupamba moto, baada ya Chama cha Wananchi (CUF) jana kuungana na wadau wengine, kuitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) kutamka wazi kuwa mchakato huo hauwezekani kufanyika katika tarehe hiyo.
Pia kimemtaka Rais Jakaya Kikwete kuwaweka wazi Watanzania juu ya kile anachotaka kuwafanya kutokana na kura hiyo kulazimishwa, huku kukiwa hakuna maandalizi yoyote ya kufanikisha kufanyika kwake.
Naibu Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CUF, Abdul Kambaya (pichani), alisema jijini Dar es Salaam jana kuwa wanataka Nec ifanye hivyo kwa kuwa wanaamini uandikishaji wapigakura katika daftari la kudumu la wapigakura, ulioanza mkoani Njombe, mwezi uliopita, kwa mfumo mpya wa BVR, hauwezi kukamilika Aprili 28 na kuwezesha kura hiyo kupigwa Aprili 30. 
Alitaja mambo yanayofanya BVR kutowezekana kukamilika mpaka tarehe hiyo kuwa ni pamoja na idadi ya watu wanaojitokeza kuzidi ile ya lengo la Nec.
Alitoa mfano wa mkoani humo, kuwa lengo la Nec lilikuwa ni kuandikisha wapigakura hadi saa 12 jioni, lakini kutokana na wingi wa watu, imejikuta ikiandikisha hadi saa 2 usiku.
“Katika mazingira haya, kuna mahali Tanzania saa 12 tu imeshakuwa usiku wa giza na umeme hakuna. Hali hii kwa vyoyote vile itatatiza utendaji na ufanisi wa mchakato huu kufanikiwa,” alisema Kambaya.
Alitaja sababu nyingine kuwa ni uwezo wa BVR kufanya kazi na kwamba, utafiti uliofanywa na maofisa wa CUF, kuna wakati mashine moja ya BVR inaandikisha chini ya watu 60 dhidi ya lengo la Nec kuandikisha 80 hadi 100 kwa siku kutokana na changamoto inazokabiliana nazo.
“Mwenyekiti wa Nec, Jaji Lubuva alipokuwa anamkaribisha Waziri Mkuu, Pinda alisema tarehe 24/2/2015 waliandikisha wapigakura 3,014 katika vituo 55. Yaani kila mashine moja ilikuwa na uwezo wa kuandikisha wastani wa wapigakura 54 kwa siku,” alisema Kambaya.
 CHANZO: NIPASHE

2 comments :

  1. Njia bora ya kutembelea wote juu ya Dubai kupitia helikopta katika billigaste sana viwango na spwcial discount. . . .
    Helicopter Tour Dubai

    ReplyDelete
  2. graet post !thanks to share with us. My Recent Post... FIFA 15 For Free

    ReplyDelete