Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, March 26, 2015

Kibao chageuka kesi ya IPTL kupinga Bunge.

Mmiliki wa IPTL, Habinder Sethi.
Kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) imejiondoa katika kesi ya kikatiba iliyoifungua Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, kupinga utekelezaji wa maazimio nane yaliyopitishwa na Bunge baada ya kushindwa kupinga mapingamizi yaliyowasilishwa na upande wa serikali. 
 
Mbali na IPTL kampuni nyingine zilizohusika kupinga maazimio hayo ni Pan Africa Power Solution Ltd (PAP) mmiliki wa IPTL, Habinder Sethi (pichani), na mmiliki wa kamapuni VIP Engineering and Marketing Ltd, James Rugemalira. 
 
Mbele ya Jaji Stella Mugasha, wakili wa upande wa utetezi, Gabriel Munyele, akisaidiana na wakili Joseph Sungwa, aliiambia mahakama kuwa hakuna haja ya kuendelea kusikiliza kesi hiyo kwani zuio la muda waliloomba lilikuwa limeshaanza kutekelezwa na Bunge. Upande wa serikali ukiongozwa na naibu Mwanasheria Mkuu, Gabriel Malata, ulidai kuwa ulipwe gharama za kesi kutokana na usumbufu uliofanywa na IPTL kung’ang’ania kupinga maazimio ambayo yalikuwa yalishaanza kutekelezwa. 
 
Malata alidai kuwa IPTL inatakiwa kulipa gharama za uendeshaji wa kesi zikiwamo uchapishaji wa majalada na muda waliotumia kuja mahakamani. 
Aidha aliiomba Mahakama itumie vifungu vya sheria vinavyoelezea na masuala ya gharama za kesi kuiamuru IPTL kulipa gharama hizo. 
 
Malata aliiomba mahakama itende haki ili kukomesha usumbufu unaofanywa na kampuni au watu wanaofungua kesi wakati wakijua hawawezi kushinda. 
 
Jaji Mugasha aliitaka kampuni ya IPTL iwajibike kwa kulipa gharama za kesi kwa kushindwa kujiondoa mapema kupinga maazimio hayo, huku wakijua fika yalishaanza kutekelezwa.
 
Wakili Malata alisisitiza kuwa upande wa serikali utafuatilia ili kuhakikisha IPTL inalipa gharama za kesi kwa wakati mwafaka. 
 
Desemba 31 mwaka jana serikali iliwasilisha mapingamizi matano katika mahakama hiyo kupinga maombi ya IPTL juu ya maazimio yaliyopitishwa na bunge. 
 
Moja ya mapingamizi ni kuwa maombi yaliyowasilishwa na IPTL hayana msingi kwa kuwa yalishaanza kutekelezwa.
 
 Pingamizi la pili IPTL hawakufungua kesi ya msingi bali walileta maombi ya kupinga utekelezaji. 
 
Mapingamizi yaliyowasilishwa na hayatekelezeki kwa kuwa hakuna vifungu vya sheria vinavyoeleza maombi waliyoomba.
 
Katika kesi hiyo namba 57 iliyosajiliwa mwaka jana IPTL ilifungua kesi ya maombi kupinga ya maazimio nane yaliyopitishwa na bunge yakiwamo. 
 
Miongoni mwa maazimio hayo ni Bunge kuitaka Takukuru, Jeshi la Polisi na vyombo vingine husika vya ulinzi na usalama kuwachukulia hatua stahiki za kisheria watu wote waliotajwa na taarifa maalumu ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC)) kuhusika na kashfa ya uchotaji wa zaidi ya Sh. bilioni 300 kutoka akaunti ya Tegeta Escrow.
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment