Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, March 10, 2015

Kigogo mwingine ajikanyaga Escrow.

Mkurugenzi Mdhibiti Uchumi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Dk. James Benedict Diu, akijitetea mbele ya Baraza la Maadili, jijini Dar es Salaam jana. 
Mkurugenzi Mdhibiti Uchumi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Dk. James Benedict Diu, amekiri kupokea mgawo wa zaidi ya Sh. milioni 80.8 kutoka kwa mmiliki wa kampuni ya VIP Engineering and Marketing Limited, James Rugemalira, huku akitoa maelezo yanayokinzana kuhusu sababu za kupewa fedha hizo pamoja na matumizi yake.
 
Fedha hizo, ambazo anadaiwa kuingiziwa na Rugemalira katika akaunti yake iliyofunguliwa katika Benki ya Biashara ya Mkombozi tawi la St. Joseph, jijini Dar es Salaam, zinadaiwa kuwa ni sehemu ya zaidi ya Sh. bilioni 200 zilizochotwa kifisadi katika akaunti ya Tegeta Escrow, iliyokuwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
 
Dk. Diu, ambaye amewahi kuwa Meneja Udhibiti wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) mwaka 2006-2011, alitoa maelezo hayo kwa nyakati tofauti wakati akijibu tuhuma za ukiukwaji wa maadili ya viongozi wa umma zinazomkabili mbele ya Baraza la Maadili jana na kudai kuwa hazijui kazi za Ewura. ADAI FEDHA NI MSAADA KUMUUGUZA MKEWE
Awali, akimhoji shahidi wa upande wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, ambao ni walalamikaji katika shauri hilo, Zahara Guga, Dk. Diu alidai fedha alizopokea kutoka kwa Rugemalira, hazikuwa zawadi, bali zilikuwa ni msaada zilizotolewa kuchangia gharama za matibabu ya mkewe, Beatrice, ambaye kwa sasa ni marehemu. 
 
“Sijapokea zawadi, bali ni mchango kama msaada wa matibabu ya mke wangu. Nasisitiza tena hii haikuwa zawadi. Natambua kwamba iwapo ningepokea zawadi ningetamka kwa afisa mas-uul (bosi wake) kwa kuwa ile haikuwa zawadi sikuona umuhimu wa kuitamka,” alidai Dk. Diu.
 
MAELEZO YAKINZANA
Wakati awali akieleza fedha hizo zikiluwa ni msaada kwa ajili ya kumuuguza mkewe. baadaye wakati akitoa maelezo ya kujitetea mbele ya baraza hilo jana, Dk. Diu alidai fedha alizopewa na Rugemalira zilikuwa ni mkopo wenye masharti nafuu, ambao walikubaliana kwa mdomo aulipe siku yoyote atakapofanikiwa.
 
Hata hivyo, alipotakiwa na Wakili wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Getrude Cyriacus, alithibitishie baraza kuhusu makubaliano hayo kati yake na Rugemalira, Dk. Diu alidai suala hilo ni kati yake na Rugemalira aliyempa mkopo huo na kwamba, haliwahusu watu wengine.
 
Wakili Getrude alimhoji kama hakuona haja na umuhimu wa kwenda na Rugemalira katika baraza kuthibitisha dai hilo, Dk. Diu alidai alitegemea Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma wangemwita.
 
Alipohojiwa na Wakili Getrude sababu za kutoenda Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kuomba kibali ili kutimiza matakwa ya sera kuhusu matibabu ya viongozi wa umma nje ya nchi, Dk. Diu alijibu alishindwa kufanya hivyo kwa kuwa kipindi hicho mgonjwa wake alikuwa katika hali mbaya, hivyo hakukuwa na muda, kwani ilihitajika haraka ya kumpeleka nchini India kwa matibabu.
 
Pia Wakili Getrude akimhoji, Dk. Diu alikiri katika maelezo aliyoyatoa chini ya kiapo mbele ya kamati ya uchunguzi ya sekretarieti hiyo kuwa fedha alizopokea kutoka kwa Rugemalira zilikuwa ni kwa ajili ya kulipia deni la nyumba, iliyoko eneo la Mbezi la mwaka 2012.
 
Hata hivyo, alidai alizitamka fedha hizo kwenye fomu yake ya rasilimali za madeni kwa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma.
 
Alidai matibabu ya mkewe yaliratibiwa na Rugemalira, kutekeleza ahadi aliyoitoa baada ya kwenda kumuona katika Hospitali ya TMJ na Sanitas, zilizoko Mikocheni, jijini Dar es Salaam alikokuwa amelazwa kwa nyakati tofauti wakati akiugua.
 
Alidai Rugemalira ni rafiki wa karibu na wa siku nyingi yeye na familia yake na kwamba, alihitimu naye Shahada ya Kwanza katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) mwaka 1982-1985.
 
Hata hivyo, alidai licha ya fedha alizopewa na Rugemalira kutumika, mkewe alifariki dunia, huku gharama zilizotumika kwa matibabu na mazishi yake zikifikia Sh. milioni 127. 
 
Alihoji uhusiano kati ya VIP Engineering and Marketing Limited, kampuni ya kufufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), suala la Escrow na TCAA na kujibiwa na Zahara kuwa kilicho wazi ni kuwa yeye (Dk. Diu) ana uhusiano na Rugemalira, ambaye alipokea kutoka kwake fedha hizo, Februari 5, mwaka jana.
 
TUHUMA ZINAZO MKABILI
Dk. Diu anatuhumiwa kukiuka maadili ya viongozi wa umma akituhumiwa kuomba fadhili za kiuchumi kutoka kwa Rugemalira, kinyume cha kifungu cha 6 (f) cha Sheria ya Maadili Viongozi wa Umma kinachomzuuia kiongozi wa umma kuomba au kupokea fadhila za kiuchumi.
 
Anadaiwa Februari, mwaka jana, alipokea jumla ya Sh. 80,850,000 kutoka kampuni ya VIP Engineering and Marketing Limited iliyokuwa na hisa ya asilimia 30 na IPTL yenye mkataba wa kuongeza uzalishaji wa umeme na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), ambalo ni shirika la umma.
 
Fedha hizo zinadaiwa kuwa ziliingizwa Februari 5, mwaka jana katika akaunti ya mlalamikiwa iliyopo kwenye benki hiyo namba 00410102642001 katika tawi hilo na kwamba, kitendo hicho ni ukiukwaji wa kifungu cha 6 (e) cha sheria hiyo, ambacho kinamzuia kiongozi wa umma kujiingiza katika mgongano wa maslahi.
 
Dk. Diu pia anadaiwa kuwa kwa kutumia wadhifa wake, alijipatia manufaa ya kifedha kinyume cha kifungu cha 12 (1) (e) cha sheria hiyo na kwamba, hakutamka fedha hizo. Alikana malalamiko hayo.
 
Wakili Getrude akihitimisha, alidai mlalamikiwa pamoja na mengine, ameshindwa pia kujitetea kuhusu dola za Marekani 10,000 na dola 25 alizopokea kutoka kampuni ya Mabibo Wines and Spirit na kampuni moja ya mafuta nchini.
 
Hivyo, akaliomba baraza kutoa adhabu dhidi yake itakayokuwa fundisho kwa viongozi wengine wa umma wenye tabia na mwenendo unaokiuka maadili ya viongozi wa umma.
 
Mwenyekiti wa Baraza hilo, Jaji Hamisi Msumi, alisema baraza litatoa uamuzi kwa njia ya mapendekezo na kuyawasilisha kwa mamlaka husika kama sheria inavyosema.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment