Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, March 27, 2015

KUTOKA BARAZA LA WAWAKILISHI ZANZIBAR!

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar Mhe Fatma Ferej akijibu maswala ya Wajumbe wa Baraza kuhusiana na Ofisi yake wakati wa Kikao cha asabuhi. cha maswali na majibu na kuwasilishwa Ripoti za Kamati za Baraza la Wawakilishi.
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakiwa katika ukumbi wa Mkutano wakifuatilia michango ikiwasilishwa katika mkutano huo
Mwakilishi wa Jimbo la Mwanakwerekwe Zanzibar Mhe Shamsi Vuai Nahodha akimsikiliza Mhe Mbaroul Wadi Mtando akisisitiza jambo wakiwa katika ukumbi wa mkutano  
Maofisa wa Wizara za Serekali ya Mapinduzi Zanzibar wakifuatilia michango ya Wajumbe wa Baraza wakichangi na kujibiwa kwa maswala waliouliza kwa Wizara husika.
 
Waandishi wa habari wa vyombo vya ZBC TV na ZBC Redio wakiwa katika ukumbi wa wageni wakiripoti shughuli za Baraza la Wawakilishi kupitia vyombo vya live.
Wajumbe wakiwa katika Ukumbi wa Mkutano katika jengo la Baraza la Wawakilishi Chukwani Zanzibar
Muonekano wa Ukumbi wa Mkutano wa Baraza la Wawakilishi wakati wa Kikao cha Mkutano huo

Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Ali Abdallah Ali akitowa kwa bwaride katika Ukumbi wa Mkutano wa Baraza la ya kuahirisha kwa mapumziko ya mchana.
Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Zanzibar Mhe Juma Duni, akisalimiana na Mkurugenzi wa Idara ya Uvuvi Zanzibar Ndg Mussa Aboud Jumbe wakiwa nje ya ukumbi wa mkutano.  
Waziri wa Fedha Zanzibar Mhe Omar Yussuf Mzee kushoto na Waziri wa Ardhi Makaazi, Nishati na Maji Mhe Ramadhani Abdalla Shabani wakitoka katika ukumbi wa mkutano baada ya kuahirishwa kwa mapumziko ya mchana. 
Mwakilishi wa Mji Mkongwe Mhe Ismail Jussa akimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar Mhe Fatma Ferej, akizungumza jambo wakiwa nje ya Ukumbi wa Baraza baada ya kuahirishwa kwa mapumziko ya mafupi ya mchana. 
Mwakilishi wa Jimbo la Ole Mhe Hamad Masoud kulia akibadilisha mawazo na Mhe Shamsi Vuai Nahodho Mwakilishi wa Jimbo la Mwanakwerekwe.  
Waheshimiwa wakibadilisha mawazo wakati wa mapumziko ya Kikao cha asubuhi kuahirishwa kutoka kushoto Mhe Mohammed Diwa Jimbo la Mpendae Mhe Machano Othman Jimbo la Chumbuni na Mhe Mahmoud Thabit Kombo Jimbo la Kiembesamaki.
Waheshimiwa wakiwa na tabasamu wakitoka katika jengo la Baraza la Wawakilishi Zanzibar
Mhe Ismail Jussa akisisitiza jambo wakati akibadilishana mawazo na Wajumbe wezake nje ya ukumbi wa mkutano wa baraza.

Kutoka baraza la Wawakilishi: Kifafa cha mimba ni miongoni mwa mambo matano yanayosababisha vifo


Na Abdulla Ali na Rahma Khamis - Maelezo

Kifafa cha Mimba ni miongoni mwa mambo matano makuu yanayosababisha vifo vya moja kwa moja vya akina mama wajawazito Nchini.

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Mahamoud Thabit Kombo wakati akijibu swali la mwakilishi wa nafasi za wanawake Mhe. Shadya Mohammed Suleiman katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani nje kidogo ya Mji wa Zanzibar aliyetaka kujua ni vipi wizara ya afya Zanzibar imejipanga kukabiliana na tatizo la vifo vya akina mama wajawazito vinavyotokea wakati wa kujifungua.

Amesema kuwa miongoni mwa mambo yanayosababisha vifo vya moja kwa moja vya akina mama ni pamoja na Kutokwa na damu nyingi kabla au baada ya kujifungua (Haemorrage), Shindikizo la damu wakati wa ujauzito (Hypertensive Disorder During Pregnancy), Uzazi kanadamizi (Obstructed Labour), Maambukizo kwenye mfumo mzima wa damu (Sepsis) ambavyo hupelekea kuharibika au utoaji wa mimba usio salama unaopelekea unaopelekea maambukizi kwenye mfumo mzima wa damu (Septic Abortion).

Amefahamisha kuwa Serikali kupitia Wizara yake imekuwa ikiwashajihisha sana akina mama kuanza kwenda vituo vya afya mapema kwa ajili ya kupima ujauzito ambapo mama mjamzito anatakiwa kuhudhuria kituo cha afya kila baada ya wiki 2 hadi Mwezi 1.

Ametanabahisha kuwa iwapo akina mama watakwenda vituo vya afya mapema itawapelekea kuvifahamu viashiario hatari kwa wakati ambavyo vitaweza kushughulikiwa na kutafutiwa ufumbuzi kwa muda muwafaka kama miongozo ya huduma ya dharura kwa akina mama na watoto wachanga inavyoeleza.
Hata hivyo Naibu huyo amewataka akina mama wajawazito kuhudhuria vituo vya afya mapema na kwa mpangilio maalum unaoshauriwa na wataalamu wa afya kwani kutasaidia kupunguza matatizo ya vifo kwa akina mama hao wakati na baada ya kujifungua.

Sambamba na hayo amesema Wizara yake inajitahidi kuongeza wafanyakazi katika vituo vya afya mbalimbali vilivyopo Nchini hususan Vijijini kwa mujibu wa hali ya kiuchumi itakavyoruhusu. 

Kutoka baraza la Wawakilishi: Wananchi wana haki ya kuwauliza wawakilishi wao


Na Abdulla Ali na Rahma Khamis - Maelezo

Wananchi wana haki ya kuwauliza Wawakilishi wao kuhusiana na Fedha wanazozipatiwa kutoka Serikalini kwa ajili ya maendeleo ya Majimbo yao.

Hayo ameyaeleza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Zanzibar Mhe. Mohamed Aboud Mohamed wakati akijibu swali la mwakilishi wa nafasi za wanawake Mhe. Shadya Mohammed Suleiman katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani nje kidogo ya Mji wa Zanzibar alipotaka kujua hatua zinazochukuliwa na Serikali kwa wale wote walioshindwa kuwasilisha ripoti zao za fedha za majimbo yao.

Amesema Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wanatakiwa kuwasilisha kwa wakati ripoti za matumizi ya fedha za Majimbo yao wanazopatiwa na Serikali ili kuimarisha maendeleo ya wananchi wao.

Aidha amekiri kuwa hadi sasa Majimbo mengi bado hayajafanya marejesho ya matumizi ya fedha za mfuko wa Mwaka wa fedha 2013/2014.

“Hata hivyo napenda kutoa pongezi zangu za dhati kwa waheshimiwa wawakilishi wa majimbo 3 ambayo ni Mtoni, Donge na Chambani pamoja na Kamati zao kwa kufanya marejesho kwa Mwaka 2013/2014 kwa wakati”, ameeleza Waziri Mohamed.

Amesema kuwa Serikali kupitia Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais inawataka waheshimiwa kutekeleza matakwa ya Sheria ili lengo lililokusudiwa kufikiwa kwa nia ya kuwaletea maendeleo wananchi katika maeneo yao.  

Vilevile Waziri huyo amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ina nia njema kwa wananchi wake na ndio maana wawakilishi wao wa majimbo wanapewa kipaombele cha kupatiwa fedha za Mfuko wa Jimbo ili ziwasaidie katika matatizo yao madogomadogo lakini kwa masikitiko makubwa wawakilishi hao wanashindwa kuwasilisha ripoti zao za fedha hizo jambo linalopelekea kurejesha nyuma maendeleo ya wananchi na Taifa kwa ujumla.

Hata hivyo amefahamisha kuwa serikali imejiwekea kuleta maendeleo katika majimbo yake yote bila ya kuangalia kuwa majimbo hayo yanaongozwa na vyama pinzani au chama tawala.

Kutoka baraza la Wawakilishi: Kuongezeka kwa Baa ni tamaa za wamiliki wa maeneo bila ya kujua athari zake


Na Abdulla Ali na Rahma Khamis Maelezo

Kuongezeka kwa biashara ya vilevi (Baa) katika mji wa Zanzibar kunatokana na tamaa za wamiliki wa maeneo kwa kuuza kiholela bila ya kujua lengo la mnunuzi na athari zinazoweza kujitokeza katika jamii.

Haya yameelezwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ Mhe. Haji Omari Kheri katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani nje kidogo ya Mji wa Zanzibar wakati akijibu swali la mwakilishi wa Jimbo la Muyuni Mhe. Jaku Hashim Ayoub alipotaka kujua kuwa Serekali imewaambia nini  wananchi wa  Jimbo la Kiembe Samaki kuhusiana na tatizo hilo.

Aidha amesema biashara ya vileo nchini Zanzibar inaendeshwa kwa kufuata Sheria ya Vileo ya 1928, ambayo ndiyo iliyoweka utaratibu wa ukataji wa leseni na adhabu kwa wanaokwenda kinyume na taratibu za leseni hizo.

Amesema kila Mwaka kabla ya kutolewa leseni mpya kwa vilabu vya vilevi (Baa) hutolewa matangazo ili wale wenye pingamizi za kuwepo kwa Baa kupeleka pingamizi zao katika mamlaka ya utoaji wa leseni na hatimaye hutakiwa kufika katika vikao vya majadiliano na wajumbe wa mahakama ya vileo.
Hata hivyo  Waziri huyo amesema pamoja na kuwepo Sheria hiyo kwa muda mrefu na kufanya kazi hadi leo bila ya kua na matatizo makubwa, hivyo niwazi kuwa inahitaji marekebisho ili iendane na hali halisi ya sasa.

Waziri Kheri ameeleza kuwa Ofisi yake imewasiliana na Tume ya Kurekebisha Sheria ili kuifanyia mapitio na kuipendekeza sheria mpya itakayowasilishwa barazani hapo kwa ajili ya kujadiliwa na hatimae kuweza kutumika kama sheria iliyo kamili mara baada ya kupitishwa na wajumbe wa Baraza hilo.

“Nashukuru Tume imeshakamilisha kazi hiyo na kutupa Rasimu ya Sheria mpya baada ya kushauriana na wahusika wengine na Ofisi yangu inaifanyia kazi na muda si mrefu Mswada wa Sheria hiyo utaletwa katika Baraza lako tukufu.”Waziri amesema.

Akifafanua kuhusiana na Baa amefahamisha kuwa Jimbo la Kiembe Samaki kwa mujibu wa kumbukumbu zilizopo Baa kumi na moja (11) ambazo zote hizo zimepewa leseni kwa mujibu wa taratibu za kisheria, na Ofisi hiyo haina taarifa za kuwepo kwa Baa ambazo hazina leseni na zinazofanya kazi ndani ya Jimbo la hilo.

Ametanabahisha kuwa kwa mujibu wa sheria hiyo adhabu ya kuendesha biashara hiyo bila ya leseni ni faini au kifungo au vyote 2 kisichozidi miezi 12 na Mahakama imepewa uwezo wa kisheria wa kufilisi vinywaji vyote vitakavyokutwa ndani ya Baa isiyo na leseni.

Waziri  Kheri amewataka wananchi pamoja na kuwaomba Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kutumia utaratibu uliowekwa kisheria kwa ajili ya kutoa malalamiko yao ili yapatiwe ufumbuzi kwa wakati na hatimae kuweza kuondokana na kero ndogondogo zinzowakabili wananchi katika makaazi yao.

No comments :

Post a Comment